Kufa na kufufuka pamoja na Kristo
1 Rum 3:5-8Tuseme nini basi? Tudumu katika dhambi ili neema izidi kuwa nyingi? 2 1 Pet 4:1Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi? 3 Gal 3:27Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? 4 Kol 2:12;1 Pet 3:21Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.