Publicidade

Romanos 6

2 1 Pet 4:1Hasha! Sisi tulioifia dhambi tutaishije tena katika dhambi? 3 Gal 3:27Hamfahamu ya kuwa sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake? 4 Kol 2:12;1 Pet 3:21Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima. 5 Flp 3:10,11Kwa maana kama mlivyounganika naye katika mfano wa mauti yake, kadhalika mtaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake; 6 Gal 5:24mkijua neno hili, ya kuwa utu wetu wa kale ulisulubishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena; 7 1 Pet 4:1kwa kuwa yeye aliyekufa amehesabiwa haki mbali na dhambi.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-