Uzima katika Roho
1 Sasa, basi, hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu. 2 Rum 3:27;7:23,24Kwa sababu sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu imeniacha huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti. 3 Yn 1:14;Flp 2:7;Mdo 13:38;15:10;Ebr 2:17;4:15Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu, kwa kumtuma Mwanawe mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi, aliihukumu dhambi katika mwili; 4 Gal 5:16,25ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi, tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho.