Pular para o conteúdo
Publicidade

Ruthu 4

14 Lk 1:58;Rum 12:15Nao wale wanawake wakamwambia Naomi, Na ahimidiwe BWANA, asiyekuacha leo ukiwa huna jamaa aliye karibu; jina lake huyu na liwe kuu katika Israeli. 15 1 Sam 1:8Naye atakurejeshea uhai wako, na kukuangalia katika uzee wako; kwa maana mkweo, ambaye akupenda, naye anakufaa kuliko watoto saba, ndiye aliyemzaa.

16 Basi Naomi akamtwaa yule mtoto, akamweka kifuani pake, akawa mlezi wake. 17 Lk 1:58,59Nao wale wanawake waliokuwa jirani zake wakampa jina, wakisema, Naomi amezaliwa mwana; wakamwita jina lake Obedi;4:17 Obedi: Maana yake ni ‘Mtumishi" au "anayehudumu’. yeye ndiye baba yake Yese, aliye baba yake Daudi.

Veja também

Rute
Ver todos os capítulos de Rute