Siku kuu ya BWANA
14 Yer 30:7;Yoe 2:1;Mal 4:5;Ufu 6:17Hiyo siku ya BWANA iliyo kuu i karibu;
I karibu, nayo inafanya haraka sana;
Naam, sauti ya siku ya BWANA;
Shujaa hulia kwa uchungu mwingi huko!
15 Siku ile ni siku ya ghadhabu,
Siku ya fadhaa na dhiki,
Siku ya uharibifu na ukiwa,
Siku ya giza na utusitusi,
Siku ya mawingu na giza kuu,
16 Yer 4:19;8:16;Hos 5:8;Amo 3:6Siku ya tarumbeta na ya kamsa,
Juu ya miji yenye maboma,
Na juu ya minara mirefu.
17 Nami nitawaletea wanadamu dhiki, hata watakwenda kama vipofu, kwa sababu wamemtenda BWANA dhambi; na damu yao itamwagwa kama mavumbi, na nyama yao kama mavi. 18 Eze 7:19;Sef 3:8Fedha yao wala dhahabu yao havitaweza kuwaokoa katika siku ile ya ghadhabu ya BWANA; bali nchi yote pia itateketezwa kwa moto wa wivu wake; maana atawakomesha watu wote wakaao katika nchi hii, naam, mwisho wa kutisha.