5 Mit 2:3-6Lakini mmoja wenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa. 6 Mk 11:24Ila na aombe kwa imani, pasipo mashaka yoyote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari linalochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku. 7 Maana mtu kama yule asidhani ya kuwa atapokea kitu kwa Bwana. 8 Mtu wa nia mbili husitasita katika njia zake zote.