Pular para o conteúdo
Publicidade

Yakobo 2:15-17,26

SRUV Swahili Revised Union Version

15 Ikiwa ndugu mwanamume au ndugu mwanamke yu uchi na kupungukiwa na riziki, 16 1 Yoh 3:17na mmoja wenu akawaambia, Nendeni zenu kwa amani, mkaote moto na kushiba, lakini asiwape mahitaji ya kimwili, yafaa nini? 17 Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake. 26 Yak 2:17Maana kama vile mwili pasipo roho umekufa, vivyo hivyo na imani pasipo matendo imekufa.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    15 Ikiwa ndugu yako au dada hana mavazi wala chakula, 16 naye mmoja wenu akamwambia, "Nenda zako kwa amani, ukaote moto na kushiba," pasipo kumpatia yale mahitaji ya mwili aliyopungukiwa, yafaa nini? 17 Vivyo hivyo, imani peke yake, kama haikuambatana na matendo, imekufa.

    26 Kama vile mwili pasipo roho umekufa, kadhalika nayo imani pasipo matendo imekufa.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    15 Ikiwa ndugu yako au dada hana mavazi wala chakula, 16 mmoja wenu akamwambia, "Enenda zako kwa amani, ukaote moto na kushiba," pasipo kumpatia yale mahitaji ya mwili aliyopungukiwa, yafaa nini? 17 Vivyo hivyo, imani peke yake kama haikuambatana na matendo, imekufa.

    26 Kama vile ambavyo mwili pasipo roho umekufa, kadhalika nayo imani pasipo matendo imekufa.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.