Aina mbili za hekima
13 Yak 2:18;1 Pet 2:12Ni nani aliye na hekima na ufahamu kwenu? Na aoneshe kazi zake kwa mwenendo wake mzuri, katika upole wa hekima. 14 Efe 4:31Lakini, mkiwa na wivu wenye uchungu na ugomvi mioyoni mwenu, msijisifu, wala msiseme uongo juu ya kweli. 15 Yak 1:5,17Hekima hiyo siyo ile ishukayo kutoka juu, bali ni ya kidunia, ya tabia ya kibinadamu, na ya kishetani. 16 Maana hapo palipo wivu na ugomvi ndipo palipo machafuko, na kila tendo baya.