Pular para o conteúdo
Publicidade

Tiago 4

Kujivuna juu ya kesho

13 Mit 27:1Haya basi, ninyi msemao, Leo au kesho tutaingia katika mji fulani na kukaa humo mwaka mzima, na kufanya biashara na kupata faida; 14 Lk 12:20;Zab 39:5,11lakini hamjui yatakayokuwako kesho. Uzima wenu ni nini? Maana ninyi ni mvuke uonekanao kwa muda mfupi tu, kisha hutoweka. 15 Mdo 18:21Badala ya kusema, Bwana akipenda, tutakuwa hai na kufanya hivi au hivi. 16 Lakini sasa mwajisifu katika majivuno yenu; kujisifu kote kwa namna hii ni kubaya. 17 Lk 12:47;Rum 14:23Basi yeye ajuaye kutenda mema, wala hayatendi, kwake huyo ni dhambi.

Veja também