4 Kum 24:14-15;Law 19:13;Mal 3:5;Isa 5:9;Ayu 31:38-40Angalieni, ujira wa wakulima waliovuna mashamba yenu, ninyi mliokosa kuwalipa kwa hila, unapiga kelele, na vilio vyao waliovuna vimeingia masikioni mwa Bwana wa majeshi.
16 Basi ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, ili mpate kuponywa. Sala yake mwenye haki ina nguvu nyingi, na hutenda mengi.
19 Gal 6:1Ndugu zangu, mtu yeyote miongoni mwenu akipotoka mbali na kweli, na kurejeshwa na mtu mwingine; 20 Mit 10:12;1 Pet 4:8;Zab 51:13jueni ya kuwa yeye amrejeshaye mwenye dhambi hadi akatoka katika njia ya upotevu, ataokoa roho ya mwenye dhambi kutoka mauti, na kufunika wingi wa dhambi.