Publicidade

João 16

7 Lakini, nawaambieni ukweli: afadhali kwenu mimi niende zangu, maana nisipokwenda Msaidizi hatakuja kwenu. Lakini nikienda, basi, nitamtuma kwenu.8 Naye atakapokuja atawathibitishia walimwengu kwamba wamekosea kuhusu dhambi, uadilifu na hukumu ya Mungu.9 Wamekosea kuhusu dhambi kwa sababu hawaniamini;10 kuhusu uadilifu, kwa sababu naenda zangu kwa Baba, nanyi hamtaniona tena;11 kuhusu hukumu kwa sababu mkuu wa ulimwengu huu amekwisha hukumiwa.

Veja também

Publicidade