Publicidade

Lucas 19

1 Yesu aliingia mjini Yeriko, akawa anapita katika njia za mji huo.2 Kulikuwa na mtu mmoja mjini, jina lake Zakayo ambaye alikuwa mkuu wa watoza ushuru tena mtu tajiri.3 Alitaka kuona Yesu alikuwa nani, lakini kwa sababu ya umati wa watu, na kwa vile alikuwa mfupi, hakufaulu.4 Hivyo, alitangulia mbio, akapanda juu ya mkuyu ili aweze kumwona Yesu, kwa maana alikuwa apitie hapo.5 Basi, Yesu alipofika mahali pale, aliangalia juu akamwambia, "Zakayo, shuka upesi, maana leo ni lazima nishinde nyumbani mwako."6 Zakayo akashuka haraka, akamkaribisha kwa furaha.7 Watu wote walipoona hayo, wakaanza kunungunika wakisema, "Amekwenda kukaa kwa mtu mwenye dhambi."8 Lakini Zakayo akasimama akamwambia Yesu, "Sikiliza Bwana! Mimi nitawapa maskini nusu ya mali yangu, na kama nimenyanganya mtu yeyote kitu, nitamrudishia mara nne."9 Yesu akamwambia, "Leo wokovu umefika katika nyumba hii, kwa vile huyu pia ni wa ukoo wa Abrahamu.10 Kwa maana Mwana wa Mtu amekuja kutafuta na kuokoa waliopotea." ic

Publicidade

Veja também

Publicidade