40 Lakini yule mhalifu mwingine akamkemea mwenzake akisema: "Wewe humwogopi Mungu hata kidogo? Wewe umepata adhabu hiyohiyo.41 Wewe na mimi tunastahili, maana haya ni malipo ya yale tuliyotenda. Lakini mtu huyu hakufanya chochote kibaya."42 Kisha akasema, "Ee Yesu! Unikumbuke wakati utakapoingia katika ufalme wako."43 Yesu akamwambia, "Nakwambia kwa hakika, leo utakuwa pamoja nami peponi."
Publicidade
Lucas 23
Veja também
Publicidade