3 "Sikilizeni! Mpanzi alikwenda kupanda mbegu.

4 Alipokuwa akipanda, nyingine zilianguka njiani, ndege wakaja wakazila.

5 Nyingine zilianguka penye mawe pasipokuwa na udongo mwingi. Mbegu hizo ziliota mara kwa kuwa udongo haukuwa na kina.

6 Jua lilipochomoza, zikachomeka; na kwa kuwa mizizi yake haikuwa na nguvu, zikanyauka.

7 Nyingine zilianguka kwenye miti ya miiba, nayo ikakua na kuzisonga, nazo hazikuzaa nafaka.

8 Nyingine zilianguka katika udongo mzuri, zikakua na kuzaa: moja punje thelathini, moja sitini na nyingine mia."

9 Kisha akawaambia, "Mwenye masikio na asikie!"