Publicidade

Mateus 17

1 Baada ya siku sita, Yesu aliwachukua Petro, Yakobo na Yohane nduguye, akaenda nao peke yao juu ya mlima mrefu.2 Huko, wakiwa wanamtazama, akageuka sura, uso wake ukangaa kama jua na mavazi yake yakawa meupe kama nuru.3 Mose na Eliya wakawatokea, wakawa wanazungumza naye.4 Hapo Petro akamwambia Yesu, "Bwana, ni vizuri sana kwamba tupo hapa! Ukipenda nitajenga vibanda vitatu: kimoja chako, kimoja cha Mose na kimoja cha Eliya."5 Alipokuwa bado anasema hivyo, wingu jeupe likawafunika, na sauti ikasikika kutoka katika hilo wingu: "Huyu ni Mwanangu mpendwa, ninayependezwa naye, msikilizeni."

Publicidade

Veja também

Publicidade