1 Kisha Roho alimwongoza Yesu mpaka jangwani ili ajaribiwe na Ibilisi.2 Akafunga siku arubaini mchana na usiku, na mwishowe akaona njaa.3 Basi, mshawishi akamjia, akamwambia, "Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate."4 Yesu akamjibu, "Imeandikwa katika Maandiko Matakatifu: Binadamu hataishi kwa mikate tu, ila kwa kila neno asemalo Mungu."5 Kisha Ibilisi akamchukua mpaka Yerusalemu, mji mtakatifu, akamweka juu ya mnara wa hekalu,6 akamwambia, "Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, jitupe chini; maana imeandikwa: Mungu atawaamuru malaika wake kwa ajili yako; watakuchukua mikononi mwao, usije ukajikwaa kwenye jiwe."7 Yesu akamwambia, "Imeandikwa pia: Usimjaribu Bwana, Mungu wako."8 Kisha Ibilisi akamchukua mpaka juu ya mlima mrefu, akamwonyesha falme zote za ulimwengu na fahari zake,9 akamwambia, "Hivi vyote nitakupa kama tu ukipiga magoti na kuniabudu."10 Hapo, Yesu akamwambia, "Nenda zako Shetani! Imeandikwa: Utamwabudu Bwana Mungu wako na kumtumikia yeye peke yake."11 Basi, Ibilisi akamwacha, na malaika wakaja, wakamhudumia.
Publicidade
Mateus 4
Veja também
Publicidade