Publicidade

Romanos 8

5 Maana, wale wanaoishi kufuatana na matakwa ya mwili, hutawaliwa na fikira za mwili. Lakini wale wanaoishi kufuatana na matakwa ya Roho Mtakatifu, hutawaliwa na fikira za Roho.6 Fikira za mwili huleta kifo; fikira za Roho huleta uzima na amani.7 Maana, mwenye kutawaliwa na fikira za mwili ni adui wa Mungu; haitii sheria ya Mungu, wala hawezi kuitii.8 Watu wanaotii matakwa ya mwili hawawezi kumpendeza Mungu.

Publicidade

Veja também

Publicidade