10 Milagres de Jesus na Bíblia: Lista com versículos e explicação
Os milagres de Jesus são muito mais do que demonstrações de poder sobrenatural; eles são sinais que confirmam sua divindade e missão. Ao longo dos Evangelhos, vemos Cristo curando enfermos, dominando a natureza e vencendo a morte.
Neste guia, selecionamos 10 milagres de Jesus na Bíblia, organizados com referências e uma breve explicação sobre o impacto espiritual de cada um deles.
Os principais milagres de Jesus nos Evangelhos
1. Transformação da Água em Vinho
Referência: João 2:1-11
Explicação: Ocorreu nas Bodas de Caná. Sendo o seu primeiro milagre público, Jesus demonstrou autoridade sobre a matéria e a natureza, revelando sua glória aos discípulos e abençoando a instituição da família.
Arusi huko Kana
Siku ya tatu kulikuwa na arusi katika mji wa Kana ya Galilaya, naye mama yake Isa alikuwepo. Isa pamoja na wanafunzi wake walikuwa wamealikwa arusini pia. Divai ilipokwisha, mama yake Isa akamwambia, "Wameishiwa na divai."
Isa akamwambia, "Mama, kwa nini unanihusisha? Saa yangu haijawadia."
Mama yake akawaambia wale watumishi, "Fanyeni lolote atakalowaambia."
Basi hapo palikuwa na mitungi sita iliyotengenezwa kwa mawe; iliwekwa hapo kwa ajili ya desturi ya Kiyahudi ya kujitakasa; kila mtungi ungeweza kuchukua vipipa viwili au vitatu.
Isa akawaambia wale watumishi, "Ijazeni hiyo mitungi maji." Nao wakaijaza ile mitungi hadi juu.
Kisha akawaambia, "Sasa choteni hayo maji kidogo; mpelekeeni mkuu wa sherehe."
Hivyo wakachota, wakampelekea. Yule mkuu wa sherehe akayaonja yale maji ambayo yalikuwa yamebadilishwa kuwa divai. Hakujua divai hiyo ilikotoka ingawa wale watumishi waliochota yale maji walifahamu. Basi akamwita bwana arusi kando, akamwambia, "Watu wote hutoa divai nzuri kwanza, kisha huleta ile divai hafifu wageni wakisha kunywa sana; lakini wewe umeiweka ile nzuri zaidi hadi sasa."
Huu ndio muujiza wa kwanza wa Isa; aliufanya huko Kana ya Galilaya. Hivyo Isa alidhihirisha utukufu wake, nao wanafunzi wake wakamwamini.
2. Cura do cego de nascença
Referência: João 9:1-12
Explicação: Jesus usa lodo para curar um homem que nunca havia enxergado. Este milagre prova que Ele é a Luz do Mundo e tem poder para restaurar o que nasceu com defeito.
Isa amponya mtu aliyezaliwa kipofu
Isa alipokuwa akipita, akamwona mtu aliyekuwa kipofu tangu kuzaliwa. Wanafunzi wake wakamuuliza, "Mwalimu, ni nani aliyetenda dhambi; ni huyu mtu au wazazi wake hata azaliwe kipofu?"
Isa akawajibu, "Huyu mtu wala wazazi wake hawakutenda dhambi. Alizaliwa kipofu ili kazi za Mungu zidhihirishwe katika maisha yake. Yanipasa kuzifanya kazi zake yeye aliyenituma wakati bado ni mchana, kwa kuwa usiku waja ambapo hakuna mtu awezaye kufanya kazi. Wakati niko ulimwenguni, mimi ni nuru ya ulimwengu."
Baada ya kusema haya, akatema mate ardhini, akatengeneza tope kwa mate na kumpaka yule kipofu machoni. Kisha akamwambia, "Nenda ukanawe katika Bwawa la Siloamu" (Siloamu maana yake ni Kutumwa). Ndipo yule kipofu akaenda, akanawa, naye akarudi akiwa anaona.
Majirani zake na wale wote waliokuwa wamemwona hapo awali akiombaomba wakaanza kuuliza, "Je, huyu si yule aliyekuwa akiketi akiombaomba?" Wengine wakasema, "Ndiye."
Wengine wakasema, "Siye, bali anafanana naye."
Lakini yeye akawaambia, "Mimi ndiye."
Wakamuuliza, "Basi macho yako yalifumbuliwaje?"
Yeye akawajibu, "Yule mtu aitwaye Isa alitengeneza tope, akanipaka machoni mwangu, naye akaniambia, ‘Nenda ukanawe katika Bwawa la Siloamu,’ ndipo nikanawa nami nikapata kuona!"
Wale wakamuuliza, "Yeye huyo mtu yuko wapi?"
Akawajibu, "Sijui."
3. Multiplicação dos pães e peixes
Referência: Mateus 14:13-21
Explicação: Com apenas cinco pães e dois peixes, Jesus alimentou mais de 5 mil homens. Este sinal revela Cristo como o Pão da Vida, aquele que supre todas as nossas necessidades.
Isa alisha wanaume 5,000
Isa aliposikia yaliyokuwa yametukia, aliondoka kwa chombo akaenda mahali pasipo na watu ili awe peke yake. Lakini watu walipopata habari, wakamfuata kwa miguu kupitia nchi kavu kutoka miji. Isa alipofika kando ya bahari, aliona makundi makubwa ya watu, akawahurumia na akawaponya wagonjwa wao.
Ilipofika jioni, wanafunzi wake walienda kwake, wakamwambia, "Mahali hapa ni nyikani, na muda sasa umekwisha. Waage makundi ya watu ili waende zao vijijini wakajinunulie chakula."
Isa akawaambia, "Hakuna sababu ya wao kuondoka. Ninyi wapeni chakula."
Wakamjibu, "Tuna mikate mitano na samaki wawili tu."
Akawaambia, "Nileteeni hivyo vitu hapa." Isa akaagiza umati wa watu wakae chini kwenye nyasi. Akaichukua ile mikate mitano na wale samaki wawili, akainua macho yake akatazama mbinguni, akavibariki na kuimega ile mikate. Kisha akawapa wanafunzi, nao wanafunzi wakawagawia ule umati. Wote wakala, wakashiba. Nao wanafunzi wakakusanya vipande vilivyosalia, wakajaza vikapu kumi na viwili. Idadi ya watu waliokula walikuwa wanaume wapatao elfu tano, bila kuhesabu wanawake na watoto.
4. Jesus acalma a tempestade
Referência: Marcos 4:35-41
Explicação: Com uma ordem, o vento e o mar se aquietam. O milagre ensina sobre a paz que excede o entendimento e a autoridade do Messias sobre a criação.
Isa atuliza dhoruba
Ilipokaribia jioni ya siku hiyo, Isa akawaambia wanafunzi wake, "Tuvukeni hadi ng’ambo ya ziwa." Wakaacha umati wa watu, na wakamchukua vile alivyokuwa kwenye mashua. Palikuwa pia na mashua zingine nyingi pamoja naye. Kukawa na dhoruba kali, nayo mawimbi yakaipiga ile mashua hata ikawa karibu kujaa maji. Isa alikuwa katika shetri, akiwa analala juu ya mto. Wanafunzi wake wakamwamsha, wakamwambia, "Mwalimu, hujali kama tunazama?"
Akaamka, akaukemea ule upepo, akayaambia yale mawimbi, "Uwe kimya! Tulia!" Ule upepo ukatulia, kukawa shwari kabisa.
Isa akawaambia wanafunzi wake, "Kwa nini mnaogopa hivyo? Je, bado hamna imani?"
Nao wakawa wameogopa sana, wakaulizana, "Ni nani huyu? Hata upepo na mawimbi vinamtii!"
5. Cura da mulher com fluxo de sangue
Referência: Marcos 5:25-34
Explicação: Uma cura que aconteceu pelo toque da fé. Jesus mostra que está atento ao sofrimento individual e que a fé é o canal para receber o milagre.
Hapo palikuwa na mwanamke aliyekuwa amesumbuliwa na tatizo la kutokwa damu kwa miaka kumi na mbili. Mwanamke huyu alikuwa ameteseka sana kwa mikono ya matabibu wengi, na kutumia kila kitu alichokuwa nacho. Lakini badala ya kupona, hali yake ilizidi kuwa mbaya. Alikuwa amesikia habari za Isa, naye akaja kwa nyuma yake kwenye umati wa watu, akaligusa vazi lake, kwa maana alisema moyoni mwake, "Nikiligusa vazi lake tu, nitaponywa." Mara kutoka damu kwake kukakoma, naye akajisikia mwilini mwake amepona kabisa.
Ghafula Isa akatambua kuwa nguvu zimemtoka. Akageukia umati wa watu na kuuliza, "Ni nani aliyegusa mavazi yangu?"
Wanafunzi wake wakamjibu, "Unaona jinsi watu wanavyokusonga. Wawezaje kuuliza, ‘Ni nani aliyenigusa?’ "
Lakini Isa akaangalia pande zote ili aone ni nani aliyemgusa. Yule mwanamke, akijua kilichomtokea, akaja, akaanguka miguuni pake akitetemeka kwa hofu, akamweleza ukweli wote. Isa akamwambia, "Binti, imani yako imekuponya. Nenda kwa amani, upone kabisa ugonjwa wako."
6. Libertação do endemoninhado Gadareno
Referência: Marcos 5:1-20
Explicação: Jesus liberta um homem dominado por uma legião de espíritos. É a prova clara de sua autoridade absoluta sobre o reino das trevas.
Isa amponya mtu mwenye pepo mchafu
Isa na wanafunzi wake wakafika upande wa pili wa ziwa, wakaingia katika nchi ya Wagerasi. Isa alipotoka kwenye mashua, mara mtu mmoja mwenye pepo mchafu akatoka makaburini, akakutana naye. Mtu huyu aliishi makaburini, wala hakuna aliyeweza kumzuia hata kwa kumfunga minyororo. Kwa kuwa mara kwa mara alikuwa amefungwa minyororo mikononi na miguuni, lakini akaikata hiyo minyororo na kuzivunja zile pingu miguuni mwake. Hapakuwa na mtu yeyote aliyekuwa na nguvu za kumzuia. Usiku na mchana alikuwa makaburini na milimani, akipiga kelele na kujikatakata kwa mawe.
Alipomwona Isa kwa mbali, alimkimbilia, akapiga magoti mbele yake. Akapaza sauti kwa nguvu akisema, "Una nini nami, Isa, Mwana wa Mungu), wa kiroho, bali si wa kimwili. Aliye Juu Sana? Ninakusihi kwa jina la Mungu, usinitese!" Kwa kuwa Isa alikuwa amemwambia, "Mtoke mtu huyu, wewe pepo mchafu!"
Isa akamuuliza, "Jina lako ni nani?"
Akamjibu, "Jina langu ni Legioni, kwa kuwa tuko wengi." Akamsihi Isa sana asiwapeleke nje ya nchi ile.
Palikuwa na kundi kubwa la nguruwe lililokuwa likilisha karibu kando ya kilima. Wale pepo wachafu wakamsihi Isa wakisema, "Tuamuru twende kwenye wale nguruwe. Turuhusu tuwaingie." Basi Isa akawaruhusu, nao wale pepo wachafu wakatoka, wakawaingia hao nguruwe. Lile kundi lilikuwa na nguruwe wapatao elfu mbili, nao wote wakateremkia gengeni kwa kasi, nao wakatumbukia ziwani na kuzama.
Wale watu waliokuwa wakichunga hao nguruwe wakakimbilia mjini na vijijini kueleza yaliyotukia. Watu wakaenda kuona hayo yaliyokuwa yametukia. Walipofika kwa Isa, wakamwona yule mtu aliyekuwa amepagawa na legioni ya pepo wachafu akiwa ameketi hapo, amevaa nguo na mwenye akili timamu. Wakaogopa. Wale walioyaona mambo hayo wakawaeleza watu wengine yaliyomtokea yule mtu aliyekuwa amepagawa na pepo wachafu, na habari za lile kundi la nguruwe pia. Basi watu wakaanza kumwomba Isa aondoke katika nchi yao.
Isa alipokuwa anaingia kwenye mashua, yule mtu aliyekuwa amepagawa na pepo wachafu akamsihi Isa waende pamoja. Isa hakumruhusu, bali alimwambia, "Nenda nyumbani kwa jamaa yako ukawaeleze mambo makuu aliyokutendea Mwenyezi Mungu, na jinsi alivyokuhurumia." Yule mtu akaenda zake, akaanza kutangaza katika Dekapoli mambo makuu Isa aliyomtendea. Nao watu wote wakastaajabu.
7. Ressurreição da filha de Jairo
Referência: Marcos 5:21-43
Explicação: Jesus demonstra que a morte para Ele é como o sono. Ele restaura a vida de uma criança, trazendo esperança para uma família desesperada.
Isa amponya mwanamke na kumfufua msichana
Isa alipokwisha kuvuka tena na kufika ng’ambo, umati mkubwa wa watu wakamzunguka hapo kando ya bahari. Kisha mmoja wa viongozi wa sinagogi aliyeitwa Yairo akafika pale. Naye alipomwona Isa, akapiga magoti miguuni pake, akamsihi akisema, "Binti yangu mdogo ni mgonjwa mahututi. Tafadhali nakusihi, njoo uweke mikono yako juu yake ili apate kupona, naye ataishi." Hivyo Isa akaenda pamoja naye.
Umati mkubwa wa watu wakamfuata, nao watu wakawa wanamsonga. Hapo palikuwa na mwanamke aliyekuwa amesumbuliwa na tatizo la kutokwa damu kwa miaka kumi na mbili. Mwanamke huyu alikuwa ameteseka sana kwa mikono ya matabibu wengi, na kutumia kila kitu alichokuwa nacho. Lakini badala ya kupona, hali yake ilizidi kuwa mbaya. Alikuwa amesikia habari za Isa, naye akaja kwa nyuma yake kwenye umati wa watu, akaligusa vazi lake, kwa maana alisema moyoni mwake, "Nikiligusa vazi lake tu, nitaponywa." Mara kutoka damu kwake kukakoma, naye akajisikia mwilini mwake amepona kabisa.
Ghafula Isa akatambua kuwa nguvu zimemtoka. Akageukia umati wa watu na kuuliza, "Ni nani aliyegusa mavazi yangu?"
Wanafunzi wake wakamjibu, "Unaona jinsi watu wanavyokusonga. Wawezaje kuuliza, ‘Ni nani aliyenigusa?’ "
Lakini Isa akaangalia pande zote ili aone ni nani aliyemgusa. Yule mwanamke, akijua kilichomtokea, akaja, akaanguka miguuni pake akitetemeka kwa hofu, akamweleza ukweli wote. Isa akamwambia, "Binti, imani yako imekuponya. Nenda kwa amani, upone kabisa ugonjwa wako."
Alipokuwa bado anaongea, watu wakafika kutoka nyumbani mwa Yairo. Wakamwambia, "Binti yako amekufa. Kwa nini kuendelea kumsumbua Mwalimu?"
Aliposikia hayo waliyosema, Isa akamwambia huyo kiongozi wa sinagogi, "Usiogope. Amini tu."
Hakumruhusu mtu yeyote amfuate isipokuwa Petro, Yakobo na Yohana, nduguye Yakobo. Walipofika nyumbani mwa yule kiongozi wa sinagogi, Isa akaona ghasia, watu wakilia na kuomboleza kwa sauti kubwa. Alipokwisha kuingia ndani, akawaambia, "Kwa nini mnafanya ghasia na kulia? Mtoto hajafa, bali amelala tu." Wale watu wakamcheka.
Baada ya kuwafukuza wote nje, Isa akaenda na baba na mama wa yule mtoto, pamoja na wale wanafunzi aliokuwa nao, wakaingia ndani hadi pale alipokuwa mtoto yule. Akamshika mtoto mkono, akamwambia, "Talitha koum!" (maana yake, "Msichana, nakuambia: amka!") Mara yule msichana akasimama, akaanza kutembea (alikuwa na umri wa miaka kumi na mbili). Walipoona haya, wakastaajabu sana. Isa akawaagiza kwa ukali wasimweleze mtu yeyote jambo hilo, naye akawaambia wampe yule msichana chakula.
8. Jesus anda sobre as águas
Referência: Mateus 14:22-33
Explicação: Ao caminhar sobre o Mar da Galileia, Jesus mostra que não está sujeito às leis da física. O episódio também serve para tratar a fé e a dúvida no coração de Pedro.
Isa atembea juu ya maji
Mara Isa akawaambia wanafunzi wake waingie katika mashua wamtangulie kwenda ng’ambo ya bahari, wakati yeye alikuwa akiaga ule umati. Baada ya kuwaaga, akaenda zake mlimani peke yake kuomba. Jioni ilipofika, Isa alikuwa huko peke yake. Wakati huo ile mashua ilikuwa mbali kutoka nchi kavu ikisukwasukwa na mawimbi, kwa sababu upepo ulikuwa wa mbisho.
Wakati wa zamu ya nne ya usiku, Isa akawaendea wanafunzi wake akiwa anatembea juu ya maji. Wanafunzi wake walipomwona akitembea juu ya maji, waliingiwa na hofu kuu, wakasema, "Ni mzimu." Wakapiga yowe kwa kuogopa.
Lakini mara Isa akasema nao, akawaambia, "Jipeni moyo! Ni mimi. Msiogope."
Petro akamjibu, "Bwana Isa, ikiwa ni wewe, niambie nije kwako nikitembea juu ya maji."
Isa akamwambia, "Njoo."
Basi Petro akatoka kwenye chombo, akatembea juu ya maji kumwelekea Isa. Lakini alipoona upepo mkali aliingiwa na hofu, naye akaanza kuzama, akapaza sauti na kusema, "Bwana, niokoe!"
Mara Isa akaunyoosha mkono wake na kumshika, akamwambia, "Wewe mwenye imani haba, kwa nini uliona shaka?"
Nao walipoingia ndani ya mashua, upepo ukakoma. Ndipo wote waliokuwa ndani ya ile mashua wakamwabudu Isa, wakisema, "Hakika, wewe ndiwe Mwana wa Mungu), wa kiroho, bali si wa kimwili.."
9. Cura do paralítico
Referência: Marcos 2:1-12
Explicação: Jesus cura o corpo, mas primeiro perdoa os pecados. Este milagre estabelece que sua missão principal é a reconciliação espiritual do homem com Deus.
Isa amponya mtu aliyepooza
Baada ya siku kadhaa Isa alirudi Kapernaumu, watu wakasikia kwamba yupo nyumbani. Watu wengi wakakusanyika, kiasi kwamba hapakubaki nafasi yoyote hata mlangoni! Naye akawahubiria Neno. Ndipo baadhi ya watu wakaja wakamletea Isa mtu aliyepooza, akiwa amebebwa na watu wanne. Kwa kuwa hawakuweza kumfikisha kwa Isa kwa sababu ya umati wa watu, walitoboa tundu kwenye paa juu ya mahali Isa alikuwa, wakamshusha mtu aliyepooza akiwa amelalia mkeka wake. Isa alipoiona imani yao, alimwambia yule mtu aliyepooza, "Mwanangu, dhambi zako zimesamehewa."
Basi baadhi ya walimu wa Torati waliokuwa wameketi pale wakawaza mioyoni mwao, "Kwa nini mtu huyu anasema hivi? Huyu anakufuru! Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa Mungu peke yake?"
Mara moja Isa akatambua rohoni mwake kile walichokuwa wanawaza mioyoni mwao, naye akawaambia, "Kwa nini mnawaza hivyo mioyoni mwenu? Je, ni lipi lililo rahisi zaidi: kumwambia huyu aliyepooza, ‘Umesamehewa dhambi zako,’ au kusema, ‘Inuka, uchukue mkeka wako, uende’? Lakini ili mpate kujua kwamba Mwana wa Adamu anayo mamlaka duniani ya kusamehe dhambi": Isa akamwambia yule aliyepooza, "Nakuambia, inuka, chukua mkeka wako, uende nyumbani kwako." Yule mtu aliyekuwa amepooza akasimama, akachukua mkeka wake, akatembea machoni pao wote! Jambo hili likawashangaza wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, "Hatujapata kuona jambo kama hili kamwe!"
10. Ressurreição de Lázaro
Referência: João 11:1-44
Explicação: O milagre mais impactante antes da crucificação. Ao ressuscitar alguém morto há quatro dias, Jesus declara: "Eu sou a ressurreição e a vida".
Kifo cha Lazaro
Basi mtu mmoja, jina lake Lazaro, alikuwa mgonjwa. Yeye alikuwa akiishi Bethania, kijiji cha Mariamu na Martha dada yake. (Huyu Mariamu, ambaye Lazaro kaka yake alikuwa mgonjwa, ndiye alimpaka Bwana Isa mafuta na kuifuta miguu yake kwa nywele zake.) Hivyo hawa dada wawili walituma ujumbe kwa Isa kumwambia, "Bwana, yule umpendaye ni mgonjwa."
Lakini Isa aliposikia hayo, akasema, "Ugonjwa huu hautaleta mauti, bali ni wa kudhihirisha utukufu wa Mungu, ili Mwana wa Mungu apate kutukuzwa kutokana na ugonjwa huu." Isa aliwapenda Martha, Mariamu na Lazaro ndugu yao. Hata hivyo, baada ya kusikia kwamba Lazaro ni mgonjwa, alikawia huko alikokuwa kwa siku mbili zaidi.
Ndipo akawaambia wanafunzi wake, "Haya, turudi Yudea."
Wanafunzi wake wakamwambia, "Mwalimu, Wayahudi walikuwa wanataka kukupiga mawe, nawe unataka kurudi huko?"
Isa akawajibu, "Si kuna saa kumi na mbili za mchana katika siku moja? Wanaotembea mchana hawawezi kujikwaa, kwa maana wanaona kwa nuru ya ulimwengu huu. Lakini wale wanaotembea usiku hujikwaa kwa sababu hawana nuru ndani yao."
Baada ya kusema haya, Isa akawaambia, "Rafiki yetu Lazaro amelala, lakini naenda kumwamsha."
Wanafunzi wakamwambia, "Bwana, kama amelala usingizi ataamka." Hata hivyo, Isa alikuwa anazungumzia kuwa Lazaro amekufa, lakini wanafunzi wake hawakuelewa, walidhani kwamba anasema Lazaro amelala usingizi tu.
Kwa hiyo Isa akawaambia waziwazi, "Lazaro amekufa. Hata hivyo nafurahi kwa kuwa sikuwako huko kabla ya Lazaro kufa, ili mpate kuamini. Lakini sasa twendeni kwake."
Tomaso (aliyeitwa Pacha) akawaambia wanafunzi wenzake, "Sisi nasi twendeni tukafe pamoja naye."
Isa ndiye ufufuo na uzima
Isa alipowasili huko alikuta Lazaro amekuwa kaburini siku nne. Basi Bethania ulikuwa karibu na Yerusalemu, umbali wa yamkini maili mbili, na Wayahudi wengi walikuwa wamekuja kuwafariji Martha na Mariamu kwa ajili ya kufiwa na ndugu yao. Martha aliposikia kwamba Isa anakuja, alitoka kwenda kumlaki, ila Mariamu alibaki nyumbani.
Martha akamwambia Isa, "Bwana, kama ungekuwa hapa, ndugu yangu hangekufa. Lakini sasa ninajua kuwa chochote utakachomwomba Mungu, atakupa."
Isa akamwambia, "Ndugu yako atafufuka."
Martha akamjibu, "Ninajua ya kuwa atafufuka wakati wa ufufuo wa wafu siku ya mwisho."
Isa akamwambia, "Mimi ndiye huo ufufuo na uzima. Yeye aniaminiye mimi, hata akifa atakuwa anaishi; na yeyote aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je, unasadiki haya?"
Martha akamwambia, "Ndiyo Bwana, ninaamini ya kuwa wewe ndiwe Al-Masihi, Mwana wa Mungu, yeye ajaye ulimwenguni."
Isa alia
Baada ya kusema haya, Martha alienda akamwita Mariamu dada yake faraghani na kumwambia, "Mwalimu yuko hapa anakuita." Mariamu aliposikia hivyo, akaondoka upesi, akaenda hadi alipokuwa Isa. Isa alikuwa hajaingia kijijini, bali alikuwa bado yuko mahali pale alipokutana na Martha. Wale Wayahudi waliokuwa pamoja na Mariamu nyumbani wakimfariji walipoona ameondoka haraka na kutoka nje, walimfuata wakidhani kwamba alikuwa anaenda kule kaburini kulilia huko.
Mariamu alipofika mahali pale Isa alipokuwa, alipiga magoti miguuni pake na kusema, "Bwana, kama ungekuwa hapa, ndugu yangu hangekufa."
Isa alipomwona Mariamu akilia na wale Wayahudi waliokuja pamoja naye pia wakilia, Isa alisikia uchungu moyoni, akafadhaika sana. Akauliza, "Mmemweka wapi?"
Wakamwambia, "Bwana, njoo upaone."
Isa akalia machozi.
Ndipo Wayahudi wakasema, "Tazama jinsi alivyompenda Lazaro!"
Lakini wengine wakasema, "Je, yule aliyefungua macho ya kipofu, hakuweza kumfanya na huyu asife?"
Isa amfufua Lazaro
Isa akafika penye kaburi akiwa amefadhaika sana kwa mara nyingine. Hilo kaburi lilikuwa pango ambalo jiwe liliwekwa kwenye ingilio lake. Isa akasema, "Liondoeni jiwe."
Martha dada yake yule aliyekuwa amekufa akasema, "Lakini Bwana, wakati huu atakuwa ananuka kwani amekwisha kuwa kaburini siku nne."
Isa akamwambia, "Sikukuambia kwamba ukiamini utauona utukufu wa Mungu?"
Kwa hiyo wakaliondoa lile jiwe kutoka kaburini. Isa akainua macho yake juu, akasema, "Baba, ninakushukuru kwa kuwa wanisikia. Ninajua ya kuwa wewe hunisikia siku zote, lakini nimesema haya kwa ajili ya watu hawa waliosimama hapa, ili wapate kuamini ya kuwa wewe umenituma."
Baada ya kusema haya, Isa akapaza sauti yake, akaita, "Lazaro, njoo huku!" Yule aliyekuwa amekufa akatoka nje, mikono yake na miguu yake ikiwa imeviringishiwa vitambaa vya kitani na leso usoni pake.
Isa akawaambia, "Mfungueni; mwacheni aende zake."
Conclusão
Os milagres de Jesus revelam sua autoridade sobre a natureza, as enfermidades, o mundo espiritual e até a morte. Eles não são apenas demonstrações de poder, mas sinais que apontam para sua identidade e missão.
Ao estudar esses milagres, é possível compreender melhor o papel de Jesus e a mensagem central do Evangelho.
Se este conteúdo ajudou você a entender os milagres de Jesus na Bíblia, compartilhe este artigo para que mais pessoas também conheçam esses ensinamentos.