A última palavra vem do Senhor
A última palavra pertence ao Senhor. Os planos do homem estão sujeitos à soberania de Deus. Ele rege toda a história e nenhum de seus propósitos pode ser frustrado.
Mipango ya moyoni ni ya mwanadamu,
bali jibu la ulimi hutoka kwa Mwenyezi Mungu.
Mwenyezi Mungu hufanya kila kitu kwa kusudi lake mwenyewe;
hata waovu kwa siku ya maangamizi.
Mungu si mtu, hata aseme uongo,
wala yeye si mwanadamu, hata ajute.
Je, anasema, kisha asitende?
Je, anaahidi, asitimize?
Mwenyezi Mungu akamjibu Musa, "Je, mkono wa Mwenyezi Mungu ni mfupi sana? Sasa utaona kama jambo nililolisema litatimizwa kwa ajili yako au la."
ndivyo lilivyo neno langu litokalo kinywani mwangu:
Halitanirudia tupu,
bali litatimiliza lile nililokusudia,
na litafanikiwa katika kusudi lile nililolituma.
"Mimi ndimi Mwenyezi Mungu, Mungu wa wote wenye mwili. Je, kuna jambo lolote lililo gumu nisiloliweza?
"Ninajua ya kuwa unaweza kufanya mambo yote,
wala hakuna mpango wako unaoweza kuzuilika.
Mwenyezi Mungu hufanya lolote apendalo,
mbinguni na duniani,
katika bahari na vilindi vyake vyote.
Yeye alikuwako kabla ya vitu vyote, na katika yeye vitu vyote vinashikamana pamoja.
Mbingu na nchi zitapita, lakini maneno yangu hayatapita kamwe.
Hili jambo linakuja! Hakika litatendeka, asema Bwana Mungu Mwenyezi. Hii ndiyo siku ile niliyosema habari zake.
Lakini hamjui hata litakalotukia kesho. Maisha yenu ni nini? Ninyi ni ukungu ambao huonekana kwa kitambo kidogo kisha hutoweka. Badala yake, inawapasa kusema, "Kama Mwenyezi Mungu akipenda, tutaishi na kufanya hili ama lile."