Publicidade

Agradecimento a Deus

Por Bíblia Online

Agradecer a Deus é louvor, adoração e reconhecimento da sua soberania. Dai graças ao Senhor porque Ele é bom — a sua misericórdia dura para sempre!

Tuje mbele zake kwa shukrani,

tumtukuze kwa vinanda na nyimbo.

Ingieni malangoni mwake kwa shukrani

na katika nyua zake kwa kusifu,

mshukuruni yeye na kulisifu jina lake.

Wema wa Mwenyezi Mungu kwa watu wake

Msifuni Mwenyezi Mungu..

Mshukuruni Mwenyezi Mungu, kwa kuwa ni mwema;

fadhili zake zadumu milele.

Wewe ni Mungu wangu, nitakushukuru,

wewe ni Mungu wangu, nitakutukuza.

Mwimbieni Mwenyezi Mungu kwa shukrani,

mpigieni Mungu wetu kinubi.

Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo,

nami nitamtukuza kwa kumtolea shukrani.

Mwenyezi Mungu ni nguvu zangu na ngao yangu,

moyo wangu umemtumaini yeye,

nami nimesaidiwa.

Moyo wangu unarukaruka kwa furaha

nami nitamshukuru kwa wimbo.

Sasa, Mungu wetu, tunakushukuru

na kulisifu Jina lako tukufu.

Msijisumbue kwa jambo lolote, bali katika kila jambo kwa kuomba na kusihi pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.

Shukrani na maombi

Ninamshukuru Mungu wangu kila niwakumbukapo ninyi.

Lolote mfanyalo, ikiwa ni kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Isa, mkimshukuru Mungu Baba Mwenyezi kupitia kwake.

Shukrani kwa ajili ya imani ya Wathesalonike

Siku zote tunamshukuru Mungu kwa ajili yenu ninyi nyote, tukiwataja kwenye maombi yetu daima. Tunaikumbuka daima kazi yenu ya imani mbele za Mungu aliye Baba yetu, taabu yenu katika upendo na saburi yenu ya tumaini katika Bwana wetu Isa Al-Masihi.

Shukrani

Ninamshukuru Mungu siku zote kwa ajili yenu kwa sababu ya neema yake mliyopewa katika Al-Masihi Isa.

Lakini Mungu apewe shukrani, yeye atupaye ushindi kupitia kwa Bwana wetu Isa Al-Masihi.

Lakini Mungu apewe shukrani, yeye ambaye siku zote hutufanya tuandamane kwa ushindi tukiwa ndani ya Al-Masihi. Naye kupitia kwetu hueneza kila mahali harufu nzuri ya kumjua yeye.

Yeye ampaye mpanzi mbegu ya kupanda, na mkate uwe chakula, atawapa na kuzizidisha mbegu zenu za kupanda na kuongeza mavuno ya haki yenu. Mtatajirishwa kwa kila namna ili mpate kuwa wakarimu kila wakati, na kupitia kwetu ukarimu wenu utamletea Mungu shukrani.

Msemezane ninyi kwa ninyi kwa zaburi, nyimbo na tenzi za rohoni, mkimwimbia na kumsifu Bwana Isa mioyoni mwenu, siku zote mkimshukuru Mungu Baba Mwenyezi kwa kila jambo katika Jina la Bwana wetu Isa Al-Masihi.

Nyenyekeaneni ninyi kwa ninyi kutokana na kumcha Al-Masihi.

Isa akaichukua ile mikate mitano na wale samaki wawili, akainua macho yake akatazama mbinguni, akavibariki na kuimega ile mikate. Kisha akawapa wanafunzi wake ili wawagawie wale watu wote. Pia akawagawia wote wale samaki wawili. Watu wote wakala, wakashiba. Nao wanafunzi wake wakakusanya vipande vilivyosalia vya mikate na samaki, wakajaza vikapu kumi na viwili.

Seja o primeiro
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-