Agradecimento pela família
Agradecer pela família é reconhecer a bênção mais preciosa que Deus nos concede. Os filhos são herança do Senhor — cada membro da família é presente divino a ser celebrado.
Tazama, watoto ni urithi kutoka kwa BWANA,
Uzao wa tumbo ni thawabu.
Kama mishale mkononi mwa shujaa,
Ndivyo walivyo watoto wa ujanani.
Heri mtu yule
Aliyelijaza podo lake hivyo.
Naam, hawataona aibu
Wanaposema na adui langoni.
Shukrani kwa wema wa Mungu
Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA.
Naam, vyote vilivyo ndani yangu
Vilihimidi jina lake takatifu.
Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA,
Wala usizisahau fadhili zake zote.
Hayo hatutawaficha wana wao,
Huku tukiwaambia kizazi kingine,
Sifa za BWANA, na nguvu zake,
Na mambo yake ya ajabu aliyoyafanya.
Wana wa wana ndio taji la wazee,
Na utukufu wa watoto ni baba zao.
Niliomba nipewe mtoto huyu; BWANA akanipa dua yangu niliyomwomba;
Ombi la Paulo kwa Wafilipi
Namshukuru Mungu wangu kila niwakumbukapo,
Maana ni shukrani gani tuwezayo kumlipa Mungu kwa ajili yenu, kwa furaha ile yote tunayoifurahia, kwa sababu yenu mbele za Mungu wetu;
Mpeni BWANA, enyi jamaa za watu,
Mpeni BWANA utukufu na nguvu.
Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeukageuka.
Kwa kuwa katika utimilifu wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema.
Nao wale wanawake wakamwambia Naomi, Na ahimidiwe BWANA, asiyekuacha leo ukiwa huna jamaa aliye karibu; jina lake huyu na liwe kuu katika Israeli. Naye atakurejeshea uhai wako, na kukuangalia katika uzee wako; kwa maana mkweo, ambaye akupenda, naye anakufaa kuliko watoto saba, ndiye aliyemzaa.
Aliye hai, naam, aliye hai, ndiye atakayekusifu, kama mimi leo;
Baba atawajulisha watoto uaminifu wako.