Agradecimento pela vida
Agradecer pela vida é reconhecer que cada respiração é dom de Deus. Toda criatura que tem fôlego louve ao Senhor — porque Ele nos formou e nos sustenta com amor.
Kila chenye pumzi na kimsifu Mwenyezi Mungu.
Msifuni Mwenyezi Mungu!
Kumsifu Mwenyezi Mungu mwokozi
Msifuni Mwenyezi Mungu!.
Ee nafsi yangu, umsifu Mwenyezi Mungu,
Nitamsifu Mwenyezi Mungu maisha yangu yote;
nitamwimbia Mungu wangu sifa
wakati wote ningali hai.
Kwa maana wewe ndiwe uliyeumba utu wangu wa ndani;
uliniunga pamoja tumboni mwa mama yangu.
Ninakusifu kwa sababu nimeumbwa
kwa namna ya ajabu na ya kutisha;
kazi zako ni za ajabu,
ninajua hayo kikamilifu.
Umbile langu halikufichika kwako,
nilipoumbwa mahali pa siri.
Nilipoungwa pamoja kwa ustadi katika vilindi vya nchi,
macho yako yaliniona kabla mwili wangu haujakamilika.
Siku zangu zote ulizonipangia
ziliandikwa katika kitabu chako
kabla haijakuwa hata moja.
Nitamwimbia Mwenyezi Mungu maisha yangu yote;
nitaimba sifa kwa Mungu wangu muda wote ninaoishi.
Kutafakari kwangu na kumpendeze yeye,
ninapofurahi katika Mwenyezi Mungu.
Jueni kwamba Mwenyezi Mungu ndiye Mungu.
Yeye ndiye alituumba, sisi tu mali yake;
sisi tu watu wake,
kondoo wa malisho yake.
Ingieni malangoni mwake kwa shukrani
na katika nyua zake kwa kusifu,
mshukuruni yeye na kulisifu jina lake.
Upendo wako usiokoma
ni wa thamani mno!
Watu wakuu na wadogo
hujificha uvulini wa mabawa yako.
Wanajifurahisha katika wingi ulio nyumbani mwako,
nawe utawanywesha katika mto wa furaha zako.
Kuwa pamoja nawe ni kijito cha uzima,
katika nuru yako twaona nuru.
Maombi ya shukrani
Nitakutukuza wewe, Ee Mwenyezi Mungu,
kwa kuwa umeniinua kutoka vilindi,
na hukuacha adui zangu
washangilie juu yangu.
Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, nilikuita unisaidie
na wewe umeniponya.
Ee Mwenyezi Mungu, umenitoa Kuzimu,
umeniokoa nisishuke kwenye shimo la mauti.
Shukrani kwa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya haki yake
Ee Mwenyezi Mungu, nitakutukuza kwa moyo wangu wote,
nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu.
Nitafurahi na kushangilia ndani yako.
Nitaliimbia sifa jina lako, Ewe Uliye Juu Sana.
siku zote mkimshukuru Mungu Baba Mwenyezi kwa kila jambo katika Jina la Bwana wetu Isa Al-Masihi.
Baraka za kiroho katika Al-Masihi Isa
Ahimidiwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Isa Al-Masihi, aliyetubariki sisi kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho ndani ya Al-Masihi.
Mungu apewe shukrani kwa karama yake isiyoelezeka!
mkimshukuru Baba, ambaye amewastahilisha kushiriki katika urithi wa watakatifu katika ufalme wa nuru. Kwa maana ametuokoa kutoka ufalme wa giza na kutuingiza katika ufalme wa Mwana wake Mpendwa, ambaye kwake tunao ukombozi, yaani msamaha wa dhambi.
Ukuu wa Al-Masihi
Yeye ni mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyote. Kwake yeye vitu vyote vilivyo mbinguni na juu ya nchi viliumbwa: vitu vinavyoonekana na visivyoonekana, viwe ni viti vya utawala au falme, au wenye mamlaka au watawala; vitu vyote viliumbwa kupitia kwake na kwa ajili yake. Yeye alikuwako kabla ya vitu vyote, na katika yeye vitu vyote vinashikamana pamoja.
Mtakapokwisha kula na kushiba, msifuni Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, kwa ajili ya nchi nzuri aliyowapa.
Ee Bwana, ulichukua shauri langu,
ukaukomboa uhai wangu.
Nilizama chini sana hata pande za mwisho za milima,
makomeo ya hiyo nchi yalinifungia hata milele.
Lakini uliuleta uhai wangu kutoka shimoni,
Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wangu.
"Uhai wangu ulipokuwa unatoka,
nilikukumbuka wewe, Mwenyezi Mungu,
nayo maombi yangu yalikufikia wewe,
katika Hekalu lako takatifu.