Publicidade

Alegria e felicidade

Por Bíblia Online

A alegria é fruto do Espírito e marca do cristão. Alegrai-vos sempre no Senhor! A Bíblia ensina que a alegria de Deus é nossa fortaleza — não depende de circunstâncias, mas da presença de Deus.

Alegrai-vos no Senhor

Alegrai-vos sempre no Senhor! Outra vez digo: alegrai-vos! Na presença de Deus há plenitude de alegria eterna.

Furahini katika Bwana Isa siku zote, tena nasema furahini!

Furahini katika Bwana Isa siku zote, tena nasema furahini!

Umenijulisha njia ya uzima;

utanijaza na furaha mbele zako,

pamoja na furaha ya milele

katika mkono wako wa kuume.

Umenijulisha njia ya uzima;

utanijaza na furaha mbele zako,

pamoja na furaha ya milele

katika mkono wako wa kuume.

Nimemweka Mwenyezi Mungu mbele yangu daima.

Kwa sababu yuko mkono wangu wa kuume,

sitatikisika.

Kwa hiyo moyo wangu unafurahia,

na ulimi wangu unashangilia;

mwili wangu nao

utapumzika salama,

Lakini wote wanaokimbilia kwako na wafurahi,

waimbe kwa shangwe daima.

Ueneze ulinzi wako juu yao,

ili wale wanaolipenda jina lako

wapate kukushangilia.

Wewe ndiwe mahali pangu pa kujificha,

utaniepusha na taabu

na kunizunguka kwa nyimbo za wokovu.

Mtawala mwenye enzi yote

Pigeni makofi, enyi mataifa yote,

mpigieni Mungu kelele za shangwe!

Kwa maana Mwenyezi Mungu anapendezwa na watu wake,

anawavika wanyenyekevu taji la wokovu.

Fruto do Espírito

O fruto do Espírito é amor, alegria, paz. A alegria do Senhor é nossa fortaleza — não depende do mundo.

Lakini tunda la Roho wa Mungu ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole na kiasi. Katika mambo kama haya hakuna sheria.

Nehemia akasema, "Nendeni mkafurahie chakula kizuri na vinywaji vitamu, na mpeleke sehemu kwa wale ambao hawana chochote cha kula. Siku hii ni takatifu kwa Mwenyezi Mungu. Msihuzunike, kwa kuwa furaha ya Mwenyezi Mungu ni nguvu zenu."

Nehemia akasema, "Nendeni mkafurahie chakula kizuri na vinywaji vitamu, na mpeleke sehemu kwa wale ambao hawana chochote cha kula. Siku hii ni takatifu kwa Mwenyezi Mungu. Msihuzunike, kwa kuwa furaha ya Mwenyezi Mungu ni nguvu zenu."

Hii ndiyo siku Mwenyezi Mungu aliyoifanya,

tushangilie na kufurahi ndani yake.

Ninafurahia kufuata sheria zako

kama mtu afurahiaye mali nyingi.

Sheria zako ni urithi wangu milele,

naam ni furaha ya moyo wangu.

Thawabu ya kumtii Mwenyezi Mungu

Heri wale wote wamchao Mwenyezi Mungu,

wanaoenda katika njia zake.

Utakula matunda ya kazi yako;

baraka na mafanikio vitakuwa vyako.

Alegria nas tribulações

Os que semeiam em lágrimas ceifarão com alegria. Tende por motivo de grande gozo quando caídes em diversas tentações.

Wapandao kwa machozi

watavuna kwa nyimbo za shangwe.

Kwa maana hasira yake ni ya muda mfupi,

bali upendo wake hudumu siku zote.

Inawezekana kilio kiwepo usiku kucha,

lakini furaha huja asubuhi.

Kwa maana hasira yake ni ya muda mfupi,

bali upendo wake hudumu siku zote.

Inawezekana kilio kiwepo usiku kucha,

lakini furaha huja asubuhi.

Imani na hekima

Ndugu zangu, hesabuni kuwa ni furaha tupu mnapopatwa na majaribu mbalimbali, kwa sababu mnajua ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi.

Ingawa mtini hauchanui maua

na hakuna zabibu juu ya mizabibu,

ingawaje mzeituni hauzai,

na hata mashamba hayatoi chakula,

iwapo hakuna kondoo katika banda,

wala ng’ombe katika zizi,

hata hivyo nitashangilia katika Mwenyezi Mungu,

nitamfurahia Mungu Mwokozi wangu.

Hii ndiyo sababu nafurahia katika udhaifu, katika kutukanwa, katika taabu, katika mateso na katika shida kwa ajili ya Al-Masihi. Kwa maana ninapokuwa dhaifu, ndipo nina nguvu.

Ijapokuwa hamjamwona, mnampenda; tena ingawa sasa hammwoni, mnamwamini na kujawa na furaha yenye utukufu na isiyoelezeka. Maana mnaupokea wokovu wa roho zenu, ambao ndio lengo la imani yenu.

Ijapokuwa hamjamwona, mnampenda; tena ingawa sasa hammwoni, mnamwamini na kujawa na furaha yenye utukufu na isiyoelezeka. Maana mnaupokea wokovu wa roho zenu, ambao ndio lengo la imani yenu.

Alegria compartilhada

Alegrai-vos com os que se alegram. O Senhor fez coisas grandiosas por nós — alegrai-vos no Senhor e regozijai-vos.

Kuweni na furaha katika tumaini, katika dhiki kuweni na saburi, dumuni katika maombi.

Furahini pamoja na wenye kufurahi, lieni pamoja na wale waliao.

Kwa maana ufalme wa Mungu si kula na kunywa, bali ni haki, amani na furaha katika Roho wa Mungu.

Kwa maana ufalme wa Mungu si kula na kunywa, bali ni haki, amani na furaha katika Roho wa Mungu.

Mungu wa tumaini awajaze ninyi furaha yote na amani katika kumwamini, ili mpate kujawa na tumaini tele kwa nguvu ya Roho Mtakatifu wa Mungu.

ili kwa mapenzi ya Mungu niweze kuja kwenu kwa furaha, nami niburudishwe pamoja nanyi.

Kila mtu atoe kama anavyokusudia moyoni mwake, si kwa uchoyo au kwa kulazimishwa, kwa maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo mkunjufu.

Lakini utauwa na kuridhika ni faida kubwa.

Waagize wale ambao ni matajiri wa ulimwengu huu waache kujivuna, wala wasiweke tumaini lao katika mali ambayo si ya hakika, bali waweke tumaini lao katika Mungu ambaye hutupatia vitu vyote kwa wingi ili tuvifurahie.

Jesus e a alegria

A minha alegria esteja em vós e a vossa alegria seja completa. Pedi e recebereis para que a vossa alegria seja plena.

Nimewaambia mambo haya ili furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu iwe kamili.

Nimewaambia mambo haya ili furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu iwe kamili.

Hivyo ninyi mna maumivu sasa, lakini nitawaona tena, nayo mioyo yenu itafurahi, na furaha yenu hakuna awaondoleaye.

Hadi sasa hamjaomba jambo lolote kwa Jina langu. Ombeni nanyi mtapewa, ili furaha yenu ipate kuwa kamili.

Basi na tumtazame sana Isa mwanzilishi na mkamilishaji wa imani yetu, yeye ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake alistahimili msalaba, bila kujali aibu ya huo msalaba, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.

Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu, kwa maana yeyote anayemjia Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko na ya kuwa huwapa thawabu wale wanaomtafuta kwa bidii.

Alegria eterna

Alegria eterna terão sobre suas cabeças. O Senhor reinará com alegria sobre o seu povo para todo o sempre.

Umelikuza taifa,

na kuzidisha furaha yao,

wanafurahia mbele zako,

kama watu wanavyofurahia wakati wa mavuno,

kama mashujaa wanavyofurahia

wakigawanya nyara.

Pazeni sauti mwimbe kwa furaha, watu wa Sayuni,

kwa maana mkuu ni yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli miongoni mwenu."

waliokombolewa na Mwenyezi Mungu watarudi.

Wataingia Sayuni wakiimba;

furaha ya milele itakuwa juu ya vichwa vyao.

Watapata furaha na shangwe;

huzuni na majonzi vitakimbia.

Ninafurahia sana katika Mwenyezi Mungu,

nafsi yangu inashangilia katika Mungu wangu.

Kwa maana amenivika mavazi ya wokovu,

na kunipamba kwa joho la haki,

kama vile bwana arusi apambavyo

kichwa chake kama kuhani,

na kama bibi arusi ajipambavyo

kwa vito vyake vya thamani.

Ninafurahia sana katika Mwenyezi Mungu,

nafsi yangu inashangilia katika Mungu wangu.

Kwa maana amenivika mavazi ya wokovu,

na kunipamba kwa joho la haki,

kama vile bwana arusi apambavyo

kichwa chake kama kuhani,

na kama bibi arusi ajipambavyo

kwa vito vyake vya thamani.

Mwenyezi Mungu, Mungu wako, yu pamoja nawe,

yeye ni Shujaa mwenye nguvu anayeokoa.

Atakufurahia kwa furaha kubwa,

atakutuliza kwa pendo lake,

atakufurahia kwa kuimba."

Nenda, kula chakula chako kwa furaha, unywe divai yako kwa moyo wa shangwe, kwa maana sasa Mungu anakubali unachofanya.

Unirudishie furaha ya wokovu wako,

unipe roho ya utii, ili initegemeze.

Hakika umempa baraka za milele,

umemfanya awe na furaha

kwa shangwe ya uwepo wako.

Wasiwasi ulipokuwa mwingi ndani yangu,

faraja yako ilinipa furaha nafsini mwangu.

Mwenyezi Mungu ni nguvu zangu na ngao yangu,

moyo wangu umemtumaini yeye,

nami nimesaidiwa.

Moyo wangu unarukaruka kwa furaha

nami nitamshukuru kwa wimbo.

Tarajio la mwenye haki ni furaha,

bali matumaini ya mwovu huwa si kitu.

Mtu hupata furaha katika kutoa jibu linalofaa:

je, ni zuri namna gani neno lililotoka kwa wakati wake!

Mtu hupata furaha katika kutoa jibu linalofaa:

je, ni zuri namna gani neno lililotoka kwa wakati wake!

Baba wa mwenye haki ana furaha kubwa,

naye aliye na mwana mwenye hekima humfurahia.

Furahini siku zote; ombeni bila kukoma; shukuruni kwa kila jambo, kwa maana haya ndio mapenzi ya Mungu kwa ajili yenu katika Al-Masihi Isa.

Nawaambieni, vivyo hivyo kutakuwa na furaha zaidi mbinguni kwa sababu ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa wenye haki tisini na tisa ambao hawana haja ya kutubu.

Mfano wa hazina iliyofichwa na mfano wa lulu

"Ufalme wa mbinguni unafanana na hazina iliyofichwa shambani, ambayo mtu mmoja alipoiona akaificha tena. Kisha katika furaha yake, akaenda akauza vyote alivyokuwa navyo, akalinunua lile shamba.

Seja o primeiro
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-05_19-25-13-