Pular para o conteúdo
Publicidade

Amigo

Por Bíblia Online

O amigo verdadeiro é dádiva rara de Deus. Ele ama em todo tempo, fala a verdade em amor, aconselha com sabedoria e permanece fiel nas adversidades da vida.

Amizade verdadeira

Há amigo mais chegado que um irmão. Em todo tempo ama o amigo. O perfume e o incenso alegram o coração — assim o conselho doce do amigo.

Ajifanyiaye marafiki wengi ni kwa maangamizi yake mwenyewe;

Lakini yuko rafiki aambatanaye na mtu kuliko ndugu.

Rafiki hupenda sikuzote;

Na ndugu amezaliwa kwa siku ya taabu.

Marhamu na manukato huufurahisha moyo;

Kadhalika utamu wa rafiki ya mtu utokao katika kusudi la moyo wake.

Chuma hunoa chuma;

Ndivyo mtu aunoavyo uso wa rafiki yake.

Lawama ya wazi ni heri,

Kuliko upendo uliositirika.

Majeraha utiwazo na rafiki ni ya kweli;

Bali busu la adui ni udanganyifu.

Usimwache rafiki yako mwenyewe, wala rafiki ya baba yako,

Wala usiende nyumbani mwa ndugu yako siku ya msiba wako.

Afadhali jirani aliye karibu kuliko ndugu aliye mbali.

Nenda pamoja na wenye hekima, nawe utakuwa na hekima;

Bali rafiki wa wapumbavu ataumia.

Usifanye urafiki na mtu mwenye hasira nyingi;

Wala usiende na mtu wa ghadhabu nyingi;

Usije ukajifunza njia zake;

Na kujipatia nafsi yako mtego.

Wanadamu hutangaza kila mtu hisani yake mwenyewe;

Bali mtu aliye mwaminifu, ni nani awezaye kumpata?

Utajiri huongeza marafiki wengi;

Bali maskini hutengwa na rafiki yake.

Jesus, o amigo

Já não vos chamo servos, mas amigos. O maior amor é dar a vida pelo amigo. Jesus é o amigo que nunca falha.

Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake. Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo. Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; lakini ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu.

Amri yangu ndiyo hii, Mpendane, kama nilivyowapenda ninyi. Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake.

Wapenzi ikiwa Mungu alitupenda sisi hivi, imetupasa na sisi kupendana. Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wowote. Tukipendana, Mungu hukaa ndani yetu, na pendo lake limekamilika ndani yetu.

Katika hili tumelifahamu pendo, kwa kuwa yeye aliutoa uhai wake kwa ajili yetu; imetupasa na sisi kuutoa uhai wetu kwa ajili ya hao ndugu. Lakini mtu akiwa na riziki ya dunia, kisha akamwona ndugu yake ni mhitaji, akamzuilia huruma zake, je! Upendo wa Mungu wakaaje ndani yake huyo? Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa tendo na kweli.

Maandiko yale yakatimizwa yaliyonena, Abrahamu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa ni haki; naye aliitwa rafiki wa Mungu.

Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu;

Companheiros de fé

Dois são melhores do que um. Os companheiros de fé se fortalecem mutuamente e caminham juntos com o Senhor.

Thamani ya kuwa na rafiki

Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja;

Kwa sababu wana tuzo njema kwa kazi yao.

Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua!

Baraka za kuwa na umoja

Tazama, jinsi ilivyo vyema, na kupendeza,

Ndugu kuishi pamoja, kwa umoja.

Ni kama mafuta mazuri kichwani,

Yashukayo ndevuni, ndevu za Haruni,

Yashukayo mpaka upindo wa mavazi yake.

Ni kama umande wa Hermoni ushukao milimani pa Sayuni.

Maana huko ndiko BWANA alikoamuru baraka,

Naam, uzima hata milele.

Mimi ni mwenzi wa watu wote wakuchao,

Na wale wayatiio mausia yako.

Nao Yonathani na Daudi wakaahidiana, kwa kuwa alimpenda kama roho yake mwenyewe.

Msidanganyike; Mazungumzo mabaya huharibu tabia njema.

Seja o primeiro