Amor de casal
O amor de casal é celebrado na Bíblia como dom sagrado. O Cântico dos Cânticos exalta a beleza do amor conjugal — íntimo, exclusivo e forte como a morte.
Nitie kama mhuri moyoni mwako,
Kama mhuri juu ya mkono wako;
Kwa maana upendo una nguvu kama mauti,
Na wivu ni mkali kama ahera.
Mwako wake ni mwako wa moto,
Na miali yake ni miali ya Yahu.
Maji mengi hayawezi kuuzimisha upendo,
Wala mito haiwezi kuuzamisha;
Kama mtu angetoa badala ya upendo
Mali yote ya nyumbani mwake,
Angedharauliwa kabisa.
Umenishangaza moyo, dada yangu,
Bibi arusi, umenishangaza moyo,
Kwa mtupo mmoja wa macho yako,
Kwa mkufu mmoja wa shingo yako.
Mazungumzo ya bibi arusi na marafiki
Kubusu na anibusu kwa kinywa chake.
Maana pendo lako lapita divai;
Manukato yako yanukia vizuri;
Jina lako ni kama marhamu iliyomiminwa;
Kwa hiyo wanawali hukupenda.
Tazama, u mzuri, mpenzi wangu,
U mzuri, macho yako ni kama ya hua.
Tazama, u mzuri, mpendwa wangu,
Wapendeza, na kitanda chetu ni majani;
BWANA Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.
na ule ubavu alioutwaa katika Adamu BWANA Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu. Adamu akasema, Sasa huyu ni mfupa katika mifupa yangu, na nyama katika nyama yangu, basi ataitwa mwanamke, kwa maana ametwaliwa katika mwanamume. Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.
Apataye mke apata kitu chema;
Naye ajipatia kibali kwa BWANA.
Chemchemi yako ibarikiwe;
Nawe umfurahie mke wa ujana wako.
Ni ayala apendaye na paa apendezaye;
Matiti yake yakutoshe sikuzote;
Na kwa upendo wake ushangilie daima.
Mwanangu! Mbona unashangilia malaya,
Na kukikumbatia kifua cha mgeni?
Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe.
Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; upendo hautakabari; haujivuni; haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauhesabu mabaya; haufurahii udhalimu, bali hufurahi pamoja na kweli; huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.
Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe. Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake popote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea kanisa.
Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; wala mke asikose kumstahi mumewe.
Zaidi ya hayo yote jivikeni upendo, ndio kifungo cha ukamilifu.
Thamani ya kuwa na rafiki
Afadhali kuwa wawili kuliko mmoja;
Kwa sababu wana tuzo njema kwa kazi yao.
Kwa maana wakianguka, mmoja wao atamwinua mwenzake; lakini ole wake aliye peke yake aangukapo, wala hana mwingine wa kumwinua! Tena, wawili wakilala pamoja, hapo watapata moto; lakini mmoja aliye peke yake tu awezaje kupata moto? Hata ikiwa mtu aweza kumshinda yule aliye peke yake, wawili watamstahimili; wala kamba ya nyuzi tatu haikatiki upesi.
Hakuna mtu mmoja aliyetenda hivi, ambaye alikuwa na ufahamu kidogo. Au je! Kuna mtu mmoja atafutaye mzawa mwenye kumcha Mungu? Kwa hiyo jihadharini roho zenu; mtu awaye yote asimtende mke wa ujana wake mambo ya hiana.
Sheria mbalimbali
Mtu atwaapo mke mpya, asiende vitani pamoja na jeshi, wala asipewe shughuli juu yake yoyote; akae faragha mwaka mmoja nyumbani mwake, apate mfurahisha mkewe aliyemtwaa.