Pular para o conteúdo
Publicidade

Amor incondicional

Por Bíblia Online

O amor incondicional de Deus não depende de mérito humano. Ele nos amou quando ainda éramos pecadores. Esse amor não tem limites, não cobra preço e não pode ser perdido.

Amor sem condições

Deus prova o seu amor em que Cristo morreu por nós sendo nós ainda pecadores. O amor de Deus é gratuito e irrevogável.

Lakini Mungu anaudhihirisha upendo wake kwetu kwamba: Tulipokuwa tungali wenye dhambi, Al-Masihi alikufa kwa ajili yetu.

Hakika, ni vigumu mtu yeyote kufa kwa ajili ya mwenye haki, ingawa inawezekana mtu akathubutu kufa kwa ajili ya mtu mwema. Lakini Mungu anaudhihirisha upendo wake kwetu kwamba: Tulipokuwa tungali wenye dhambi, Al-Masihi alikufa kwa ajili yetu.

kwa kuwa wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu, wanahesabiwa haki bure kwa neema yake kupitia kwa ukombozi ulio katika Al-Masihi Isa.

Ni nani atakayetutenga na upendo wa Al-Masihi? Je, ni shida au taabu au mateso au njaa au uchi au hatari au upanga?

"Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

Sisi sote pia tuliishi katikati yao hapo zamani, tukitimiza tamaa za asili yetu ya dhambi na kufuata tamaa zake na mawazo yake. Nasi kwa asili tulistahili ghadhabu, kama watu wengine wote. Lakini Mungu kwa upendo wake mwingi kwetu sisi, ambaye ni mwingi wa rehema, hata tulipokuwa wafu kwa ajili ya makosa yetu, alitufanya tuwe hai pamoja na Al-Masihi Isa, yaani mmeokolewa kwa neema.

Lakini wema na upendo wa Mungu Mwokozi wetu ulipofunuliwa, alituokoa, si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyotenda, bali kwa sababu ya rehema zake. Alituokoa kwa kutuosha kwa kuzaliwa mara ya pili na kwa kufanywa wapya kupitia kwa Roho Mtakatifu wa Mungu, ambaye Mungu alitumiminia kwa wingi kupitia kwa Isa Al-Masihi Mwokozi wetu,

Amor eterno

Com amor eterno te amei. O amor de Deus é mais largo, mais alto e mais profundo do que podemos compreender.

Mwenyezi Mungu alitutokea zamani, akisema:

"Nimekupenda kwa upendo wa milele,

nimekuvuta kwa wema.

Mshukuruni Mungu wa mbinguni,

Fadhili zake zadumu milele.

Upendo wako, Ee Mwenyezi Mungu, unafika hadi mbinguni,

uaminifu wako hadi kwenye anga.

Rafiki hupenda wakati wote

naye ndugu amezaliwa kwa ajili ya wakati wa shida.

Hivi ndivyo Mungu alivyoonesha pendo lake kwetu: Mungu alimtuma Mwanawe wa pekee ulimwenguni, ili tupate uzima kupitia kwake.

Hili ndilo pendo: si kwamba tulimpenda Mungu, bali yeye alitupenda, akamtuma Mwanawe, ili yeye awe dhabihu ya upatanisho kwa ajili ya dhambi zetu.

Twampenda yeye kwa sababu yeye alitupenda kwanza.

Kwa namna hii twaweza kulijua pendo la Mungu: Kwa sababu Isa Al-Masihi aliutoa uhai wake kwa ajili yetu. Nasi imetupasa kuutoa uhai kwa ajili ya hao ndugu.

Amar como Deus ama

O amor é paciente e bondoso. Amai os vossos inimigos. O amor incondicional se expressa no perdão e na compaixão.

Upendo huvumilia, upendo hufadhili, upendo hauoni wivu, hauna majivuno, hauna kiburi. Haukosi kuwa na adabu, hautafuti mambo yake, haukasiriki upesi, hauweki kumbukumbu ya mabaya.

Upendo haufurahii mabaya bali hufurahi pamoja na kweli. Upendo huvumilia yote, huamini yote, hutumaini yote, hustahimili yote.

Wapendeni adui zenu

"Mmesikia kwamba ilinenwa, Mpende jirani yako na umchukie adui yako.Lakini ninawaambia: Wapendeni adui zenu, na waombeeni wanaowatesa ninyi, ili mpate kuwa watoto wa Baba yenu aliye mbinguni. Kwa maana yeye huwaangazia jua lake watu waovu na watu wema, naye huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki. Mkiwapenda tu wale wanaowapenda, mtapata thawabu gani? Je, hata watoza ushuru hawafanyi hivyo? Nanyi mkiwasalimu ndugu zenu tu, je, mnafanya nini zaidi ya wengine? Je, hata watu wasiomjua Mungu hawafanyi hivyo? Kwa hiyo kuweni wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.

Wapendeni adui zenu

"Lakini nawaambia ninyi mnaonisikia: Wapendeni adui zenu. Watendeeni mema wanaowachukia. Wabarikini wale wanaowalaani, waombeeni wale wanaowatendea mabaya.

Zaidi ya yote, dumuni katika upendo kwa maana upendo husitiri wingi wa dhambi.

Seja o primeiro