Pular para o conteúdo
Publicidade

Amor próprio

Por Bíblia Online

O amor próprio saudável reconhece o valor que Deus nos deu. Fomos criados à imagem de Deus, maravilhosamente formados. Aceitar-se é honrar o Criador.

Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa

Kwa njia ya ajabu ya kutisha.

Matendo yako ni ya ajabu,

Na nafsi yangu yajua sana,

Mawazo yako ni mazito sana kwangu;

Ee Mungu; nayo ni makuu sana.

Kama ningeyahesabu ni mengi kuliko mchanga;

Niamkapo ningali pamoja nawe.

Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako,

Mwezi na nyota ulizoziratibisha;

Mtu ni kitu gani hata umkumbuke,

Na binadamu hata umwangalie?

Umemfanya mdogo kuliko Mungu;

Umemvika taji la utukufu na heshima;

Humwinua mnyonge kutoka mavumbini,

Na kumpandisha maskini kutoka jaani.

Ili amketishe pamoja na wakuu,

Pamoja na wakuu wa watu wake.

Lakini BWANA akamwambia Samweli, Usimtazame uso wake, wala urefu wa kimo chake; kwa maana mimi nimemkataa. BWANA haangalii kama binadamu aangaliavyo; maana wanadamu huitazama sura ya nje, bali BWANA huutazama moyo.

Bali ninyi ni uzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;

Je! Shomoro watano hawauzwi kwa senti mbili? Wala hasahauliwi hata mmojawapo mbele za Mungu. Lakini hata nywele za vichwa vyenu zimehesabiwa zote. Msiogope basi, bora ninyi kuliko Shomoro wengi.

Kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia kila mtu aliyeko kwenu asinuie makuu kupita ilivyompasa kunuia; bali awe na nia ya kiasi, kama Mungu alivyomgawia kila mtu kiasi cha imani.

Seja o primeiro