Pular para o conteúdo
Publicidade

Salmos 8

Utukufu wa Mungu na hadhi ya utu

Kwa mwimbishaji: kwa kufuata Gitithi. Zaburi ya Daudi.

1 Ee, MUNGU, Bwana wetu

Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani kote!

Wewe umeuweka utukufu wako mbinguni;

2 Mt 21:16;11:25;1 Kor 1:27 Vinywani mwa watoto wachanga na wanyonyao

Umeiweka misingi ya nguvu;

Kwa sababu yao wanaoshindana nawe;

Uwakomeshe adui na mjilipiza kisasi.

3 Zab 44:16;19:1;Ayu 22:12;Rum 1:20 Nikiziangalia mbingu zako, kazi ya vidole vyako,

Mwezi na nyota ulizoziratibisha;

4 Ayu 7:17-18;Zab 144:3;Ebr 2:6-8 Mtu ni kitu gani hata umkumbuke,

Na binadamu hata umwangalie?

5 Umemfanya mdogo kuliko Mungu;

Umemvika taji la utukufu na heshima;

6 1 Kor 15:27;Efe 1:22;Ebr 2:8;Mwa 1:26 Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako;

Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake.

7 Kondoo, na ng’ombe wote pia;

Naam, na wanyama wa porini;

8 Ndege wa angani, na samaki wa baharini;

Na kila kipitacho njia za baharini.

9 Ayu 11:7;Zab 35:10 Wewe, MUNGU, Bwana wetu,

Jinsi lilivyo tukufu jina lako duniani kote!

Veja também