Usalama wa watu wa Mungu
Wimbo wa kupanda mlima.
1 Wamtumainio BWANA ni kama mlima Sayuni,
Ambao hautikisiki, wakaa milele.
2 Kama milima inavyouzunguka Yerusalemu,
Ndivyo BWANA anavyowazunguka watu wake,
Tangu sasa na hata milele.
3 Kwa maana fimbo ya udhalimu
Haitakaa juu ya nchi ya wenye haki;
Ili wenye haki wasije wakainyosha
Mikono yao kwenye upotovu.
4 Ee BWANA, uwatendee mema walio wema,
Nao walio wanyofu wa moyo.
5 Bali wao wanaozigeukia njia zao zilizopotoka,
BWANA atawaondoa pamoja na watenda maovu.
Amani ikae na Israeli.