Pular para o conteúdo
Publicidade

Zaburi 137

Maombolezo juu ya maangamizi ya Yerusalemu

1 Eze 1:1;Dan 8:2;Isa 24:8;Omb 5:15;Amo 8:10;Ufu 18:22 Kando ya mito ya Babeli ndiko tulikoketi,

Tukalia tulipoikumbuka Sayuni.

2 Katika miti iliyo katikati yake

Tulivitundika vinubi vyetu.

3 Maana huko waliotuchukua mateka

Walitaka tuwaimbie;

Na waliotuonea walitaka tuwatumbuize;

Tuimbieni baadhi ya nyimbo za Sayuni.

4 Twawezaje kuimba wimbo wa BWANA

Katika nchi ya ugeni?

5 Nikikusahau, Ee Yerusalemu,

Mkono wangu wa kulia na upooze.

6 Eze 3:26 Ulimi wangu na ugandamane

Na kaakaa la kinywa changu, nisipokukumbuka.

Nisipoikuza Yerusalemu

Zaidi ya furaha yangu iliyo kuu.

7 Omb 4:22;Oba 1:10 Ee BWANA, uwakumbuke wana wa Edomu,

Siku ile Yerusalemu ilipotekwa.

Kwa namna walivyosema, Bomoeni!

Bomoeni hata misingini!

8 Isa 13:1;Ufu 18:6 Ee binti Babeli, uliye karibu na kuangamia,

Heri atakayekupatiliza, ulivyotupatiliza sisi.

9 Heri yeye atakayewakamata wadogo wako,

Na kuwaseta wao juu ya mwamba.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também