Nyumba ya mwumini yenye furaha
Wimbo wa kupanda mlima.
1 Heri kila mtu amchaye BWANA,
Aendaye katika njia yake.
2 Taabu ya mikono yako hakika utaila;
Utakuwa heri, na kwako kwema.
3 Mkeo atakuwa kama mzabibu uzaao,
Katika nyumba yako.
Wanao watakuwa kama miche ya mizeituni
Wakiizunguka meza yako.
4 Tazama, atabarikiwa hivyo, yule amchaye BWANA.
5 BWANA akubariki toka Sayuni;
Uone uheri wa Yerusalemu siku zote za maisha yako;
6 Naam, ukawaone wana wa wanao.
Amani ikae na Israeli.