Sala ya kuponywa ugonjwa hatari
Kwa mwimbishaji: kwa ala za muziki zenye nyuzi; kulingana na mtindo wa Sheminithi. Zaburi ya Daudi.
1 Zab 38:1 BWANA, usinikemee kwa hasira yako,
Wala usinirudi kwa ghadhabu yako.
2 Hos 6:1 BWANA, unifadhili, maana ninanyauka;
BWANA, uniponye, mifupa yangu imefadhaika.
3 Mit 18:14;Mt 26:38 Na nafsi yangu imefadhaika sana;
Na Wewe, BWANA, hadi lini?
4 BWANA urudi, uniopoe nafsi yangu,
Uniokoe kwa ajili ya fadhili zako.
5 Zab 30:9 Maana mautini hapana kumbukumbu lako;
Katika kuzimu ni nani atakayekushukuru?
6 Nimechoka kwa kuugua kwangu;
Kila usiku nakibubujikia kitanda changu;
Nililowesha godoro langu kwa machozi yangu.
7 Macho yangu yameharibika kwa masumbufu,
Na kuchakaa kwa sababu yao wanaoniudhi.
8 Mt 7:23;Lk 13:27 Ondokeni kwangu, ninyi nyote mtendao uovu;
Kwa kuwa BWANA ameisikia sauti ya kilio changu.
9 Zab 3:4;31:22;40:1,2 BWANA ameisikia dua yangu;
BWANA atayatakabali maombi yangu.
10 Adui zangu wote wataaibika na kufadhaika,
Watarudi nyuma, kwa ghafla wataaibika.