Publicidade

Salmos 142

Sala ya ukombozi kutoka kwa watesi
Utenzi wa Daudi. Alipokuwa pangoni. Ombi.

1 Kwa sauti yangu nitamlilia BWANA,

Kwa sauti yangu nitamwomba BWANA dua.

2 Nitafunua mbele zake malalamiko yangu,

Shida yangu nitaitangaza mbele zake.

3 Roho yangu inapozimia unayajua mapito yangu;

Katika njia niendayo wamenifichia mtego.

4 Utazame mkono wangu wa kulia ukaone,

Kwa maana sina mtu anijuaye.

Makimbilio yamenipotea,

Hakuna wa kunitunza roho.

5 BWANA, nimekuita nikasema, Ndiwe kimbilio langu,

Fungu langu katika nchi ya walio hai.

6 Ukisikilize kilio changu,

Kwa maana nimedhilika sana.

Uniponye kutoka kwa wanaonifuatia,

Kwa maana wao ni hodari kuliko mimi.

7 Uitoe nafsi yangu kifungoni.

Nipate kulishukuru jina lako.

Wenye haki watanizunguka,

Kwa kuwa Wewe unanikirimu.

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-16_06-50-08-