Publicidade

Salmos 143

Sala ya ukombozi kutoka kwa adui
Zaburi ya Daudi.

1 Ee BWANA, uisikie sala yangu, uzisikilize dua zangu Unijibu Kwa uaminifu wako,

Unijibu kwa haki yako.

2 Wala usimhukumu mtumishi wako,

Maana kwako hakuna aliye hai mwenye haki.

3 Maana adui ameifuatia nafsi yangu,

Ameutupa chini uzima wangu.

Amenikalisha mahali penye giza,

Kama watu waliokufa zamani.

4 Na roho yangu imezimia ndani yangu,

Moyo wangu ndani yangu umeshtuka.

5 Nimezikumbuka siku za kale,

Nimeyatafakari matendo yako yote,

Naziwaza kazi za mikono yako.

6 Nakunyoshea mikono yangu;

Nafsi yangu inakuonea kiu kama nchi kame.

7 Ee BWANA, unijibu hima, roho yangu imelegea;

Usinifiche uso wako,

Nisifanane nao washukao shimoni.

8 Uniwezeshe kusikia fadhili zako asubuhi,

Kwa maana nimekutumaini Wewe.

Unifundishe njia nitakayoiendea,

Kwa maana ninakuinulia nafsi yangu.

9 Ee BWANA, uniponye kutoka kwa adui zangu;

Nimekukimbilia Wewe, unifiche.

10 Unifundishe kuyatenda mapenzi yako,

Kwa maana ndiwe Mungu wangu;

Roho yako mwema aniongoze katika njia iliyo sawa,

11 Ee BWANA, uniponye kwa ajili ya jina lako,

Kwa haki yako unitoe roho yangu taabuni;

12 Kwa fadhili zako utawakatilia mbali adui zangu;

Na kuwaangamiza wote wanitesao nafsi,

Kwa maana mimi ni mtumishi wako.

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-18_10-32-54-