Publicidade

Salmos 28

Sala ya kupata msaada na shukrani za msaada
Ya Daudi.

1 Ee BWANA, nitakuita Ewe, mwamba wangu,

Usiwe kwangu kama kiziwi.

Nisije nikafanana nao washukao shimoni,

Ikiwa umeninyamalia.

2 Uisikie sauti ya dua yangu nikuombapo,

Nikipainulia patakatifu pako mikono yangu.

3 Usinikokote pamoja na wasio haki,

Wala pamoja na watenda maovu.

Wawaambiao jirani zao maneno ya amani,

Lakini mioyoni mwao mna madhara.

4 Uwape sawasawa na vitendo vyao,

Na kwa kadiri ya uovu wa matendo yao,

Uwape sawasawa na kazi ya mikono yao,

Uwalipe kile wanachostahili.

5 Maana hawazifahamu kazi za BWANA,

Wala matendo ya mikono yake,

Atawavunja wala hatawajenga tena;

6 Na ahimidiwe BWANA.

Maana ameisikia sauti ya dua yangu;

7 BWANA ni nguvu zangu na ngao yangu.

Moyo wangu umemtumaini,

Nami nimesaidiwa;

Basi, moyo wangu unashangilia,

Na kwa wimbo wangu nitamshukuru.

8 BWANA ni nguvu za watu wake,

Naye ni ngome ya wokovu kwa masihi wake.

9 Uwaokoe watu wako, uubariki urithi wako,

Uwachunge, uwachukue milele.

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-16_06-50-08-