Publicidade

Salmos 70

Sala ya ukombozi kutoka kwa adui
Kwa mwimbishaji. Ya Daudi, kama matoleo ya ukumbusho.

1 Ee Mungu, uniokoe,

Ee BWANA, unisaidie hima.

2 Waaibike, wafedheheke,

Wanaoitafuta nafsi yangu.

Warudishwe nyuma, watahayarishwe,

Wapendezwao na shari yangu.

3 Warudi nyuma, na iwe aibu yao,

Wanaosema, Ewe! Ewe!

4 Washangilie, wakufurahie,

Wote wakutafutao.

Waupendao wokovu wako

Waseme daima, Atukuzwe Mungu.

5 Nami ni maskini na mhitaji,

Ee Mungu, unijilie kwa haraka.

Ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu,

Ee BWANA, usikawie.

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-16_18-40-07-