Publicidade

Salmos 1

KITABU CHA KWANZA

Njia mbili

1 Heri mtu yule asiyekwenda

Katika shauri la wasio haki;

Wala hakusimama katika njia ya wenye dhambi;

Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.

2 Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo,

Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.

3 Naye atakuwa kama mti uliopandwa

Kandokando ya vijito vya maji,

Uzaao matunda yake kwa majira yake,

Wala jani lake halinyauki;

Na kila alitendalo litafanikiwa.

4 Sivyo walivyo wasio haki;

Hao ni kama makapi yapeperushwayo na upepo.

5 Kwa hiyo wasio haki hawatasimama hukumuni,

Wala wakosaji katika kusanyiko la wenye haki.

6 Kwa kuwa BWANA anaijua njia ya wenye haki,

Bali njia ya wasio haki itapotea.

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-15_21-32-39-