Pular para o conteúdo
Publicidade

Zaburi 87

Shangwe ya kuishi Sayuni

Ya Wakorahi. Zaburi. Wimbo.

1 Msingi wake upo

Juu ya milima mitakatifu.

2 BWANA ayapenda malango ya Sayuni

Kuliko maskani zote za Yakobo.

3 Isa 60:1 Mambo makuu yanasemwa kukuhusu,

Ee Mji wa Mungu.

4 Nitataja Rahabu na Babeli

Miongoni mwao wanaonijua.

Tazama Filistia, na Tiro, na Kushi;

Wanasema, Huyu alizaliwa humo.

5 Eze 48:35;Mt 16:18 Naam, kuhusu Sayuni yatasemwa,

Huyu na huyu alizaliwa humo.

Na Yeye Aliye Juu

Atauimarisha.

6 Zab 22:30;Isa 4:3;Yer 3:19;Eze 13:9 BWANA ataweka kumbukumbu, awaandikapo mataifa,

Huyu alizaliwa humo.

7 Waimbao na wachezao ngoma na waseme,

Visima vyangu vyote vimo mwako.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também