Publicidade

Salmos 136

Uumbaji wa Mungu na matukio ya kihistoria

1 Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

2 Mshukuruni Mungu wa miungu;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

3 Mshukuruni Bwana wa mabwana;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

4 Yeye peke yake afanya maajabu makuu;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

5 Yeye aliyeumba mbingu kwa fahamu zake;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

6 Yeye aliyeitandaza nchi juu ya maji;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

7 Yeye aliyeumba mianga mikubwa;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

8 Jua litawale mchana;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

9 Mwezi na nyota zitawale usiku;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

10 Yeye aliyewapiga Wamisri kwa kuwaua wazaliwa wao wa kwanza;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

11 Akawatoa Waisraeli katikati yao;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

12 Kwa mkono hodari na mkono ulionyoshwa;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

13 Yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

14 Akawavusha Israeli katikati yake;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

15 Akamwangusha Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

16 Yeye aliyewaongoza watu wake jangwani;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

17 Yeye aliyewapiga wafalme wakuu;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

18 Akawaua wafalme mashuhuri;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

19 Sihoni, mfalme wa Waamori;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

20 Na Ogu, mfalme wa Bashani;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

21 Akaitoa nchi yao iwe urithi;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

22 Urithi wa Israeli mtumishi wake;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

23 Aliyetukumbuka katika unyonge wetu;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

24 Akatuokoa na watesi wetu;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

25 Yeye akipaye kila kiumbe chakula chake;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

26 Mshukuruni Mungu wa mbingu;

Kwa maana fadhili zake ni za milele.

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-16_18-40-07-