Wimbo wa arusi ya kifalme
Kwa mwimbishaji: kwa kufuata mtindo wa Yungiyungi. Wimbo wa Wakorahi; Wimbo wa Mapenzi.
1 Moyo wangu umefurika kwa jambo jema,
Mimi nasema niliyomfanyia mfalme;
Ulimi wangu ni kama kalamu ya mwandishi stadi.
2 Wewe u mzuri sana kuliko wanadamu;
Neema imemiminiwa midomoni mwako,
Kwa hiyo Mungu amekubariki hata milele.
3 Jifungie upanga wako pajani, wewe uliye hodari,
Utukufu ni wako na fahari ni yako.
4 Katika fahari yako usitawi uendelee
Kwa ajili ya kweli, upole na haki
Na mkono wako wa kulia
Utakutendea mambo ya ajabu.
5 Mishale yako ni mikali, katika mioyo ya adui za mfalme;
Watu huanguka chini yako.
6 Ebr 1:8-9;Zab 93:2;Isa 9:6,7 Kiti chako cha enzi, Mungu, ni cha milele na milele,
Fimbo ya ufalme wako ni fimbo ya adili.
7 Zab 33:5;Mt 3:15;Ebr 1:9;Isa 61:1;Yn 20:17 Umeipenda haki;
Umeichukia dhuluma.
Kwa hiyo MUNGU, Mungu wako, amekutia mafuta,
Mafuta ya furaha kuliko wenzako.
8 Mavazi yako yote hunukia manemane
Na udi na mdalasini.
Katika majumba ya pembe
Vinubi vimekufurahisha.
9 Binti za wafalme wamo
Miongoni mwa akina bibi wako wastahiki.
Katika mkono wako wa kulia amesimama malkia
Akiwa amevaa dhahabu safi ya Ofiri.
10 Kum 21:13 Sikia, binti, utazame, utege sikio lako,
Uwasahau watu wako na nyumba ya baba yako.
11 Zab 95:6;Isa 54:5 Naye mfalme atautamani uzuri wako,
Maana ndiye bwana wako, nawe umsujudie.
12 Na watu wa Tiro45:12 Katika Kiebrania ni binti Tiro. wanakushawishi kwa zawadi,
Nao matajiri wa watu watajipendekeza kwako.
13 Ufu 19:7,8 Binti mfalme yumo ndani ana fahari tupu,
Mavazi yake ni ya nyuzi za dhahabu.
14 Anapelekwa kwa mfalme
Na mavazi yaliyofumwa kwa uzuri.
Wanawali wenzake wanaomfuata,
Pia watapelekwa kwako.
15 Watapelekwa kwa furaha na shangwe,
Na kuingia katika nyumba ya mfalme.
16 1 Pet 2:9;Ufu 1:6 Badala ya baba zako watakuwapo watoto wako,
Utawafanya kuwa wakuu katika nchi zote.
17 Isa 11:10;Mal 1:11 Jina lako nitalifanya kuwa kumbukumbu
Katika vizazi vyote.
Kwa hiyo mataifa watakushukuru
Milele na milele.