Publicidade

Salmos 48

Utukufu wa nguvu za Sayuni
Wimbo. Zaburi ya Wakorahi.

1 Bwana ndiye aliye mkuu,

Na mwenye kusifiwa sana.

Katika mji wa Mungu wetu,

Katika mlima wake mtakatifu.

2 Kuinuka kwake ni mzuri sana,

Ni furaha ya dunia yote.

Mlima Sayuni, kule upande wa kaskazini,

Mji wa Mfalme mkuu.

3 Mungu katika majumba yake

Amejijulisha kuwa ngome.

4 Maana, tazama, wafalme walikusanyika;

Walikuja wote pamoja.

5 Mara Walipouona, wakashtuka;

Wakafadhaika na kukimbia.

6 Papo hapo tetemeko liliwashika,

Uchungu kama wa mwanamke azaaye.

7 Kama upepo wa mashariki

Unapovunja jahazi za Tarshishi.

8 Kama tulivyosikia, ndivyo tulivyoona,

Katika mji wa BWANA wa majeshi.

Mji wa Mungu wetu;

Mungu atauimarisha hata milele.

9 Tumezitafakari fadhili zako, Ee Mungu,

Katikati ya hekalu lako.

10 Kama lilivyo jina lako, Ee Mungu,

Ndivyo na sifa yako hadi miisho ya dunia.

Mkono wako wa kulia umejaa haki;

11 Na ufurahi mlima Sayuni.

Binti za Yuda na washangilie

Kwa sababu ya hukumu zako.

12 Tembeeni katika Sayuni,

Uzungukeni mji wote,

Ihesabuni minara yake,

13 Tieni moyoni boma zake,

Yafikirini majumba yake,

Mpate kuwaambia kizazi kitakachokuja.

14 Kwa maana ndivyo alivyo

MUNGU, Mungu wetu.

Milele na milele

Yeye ndiye atakayetuongoza.

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-16_18-40-07-