Pular para o conteúdo
Publicidade

Zaburi 11

Wimbo wa kumtumainia Mungu

Kwa mwimbishaji. Ya Daudi.

1 BWANA ndiye niliyemkimbilia.

Mbona mnaiambia nafsi yangu,

Kimbia kama ndege mlimani kwenu?

2 Maana, tazama, wasio haki wanaupinda uta,

Wanaitia mishale yao katika upote,

Ili kuwapiga gizani wanyofu wa moyo.

3 Kama misingi ikiharibika,

Mwenye haki atafanya nini?

4 Hab 2:20;Efe 5:13;Ebr 4:13 BWANA yu katika hekalu lake takatifu.

BWANA ambaye kiti chake kiko mbinguni,

Macho yake yanaangalia;

Kope zake zinawapima wanadamu.

5 Ayu 5:17;Zab 94:12 BWANA humjaribu mwenye haki;

Bali nafsi yake humchukia asiye haki,

Na mwenye kupenda udhalimu.

6 Awanyeshee wasio haki mitego,

Moto na kiberiti na upepo wa joto

Na viwe fungu la kikombe chao.

7 Kwa kuwa BWANA ni mwenye haki,

Apenda matendo ya haki,

Wanyofu wa moyo watauona uso wake.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também