Pular para o conteúdo
Publicidade

Zaburi 60

Sala ya ushindi wa kitaifa baada ya kushindwa

Kwa mwimbishaji: kwa kufuata mtindo wa Shushani Eduthi. Utenzi wa Daudi; wa kufundisha; wakati alipopambana na Waaramu. Kutoka Naharaimu na Zoba, na Yoabu alipowaua Waedomi 12,000 katika Bonde la Chumvi alipokuwa akirudi.

1 Ee Mungu, umetutupa na kututawanya,

Umekuwa na hasira, uturudishe tena.

2 Umeitetemesha nchi na kuipasua,

Upaponye palipobomoka, maana inatikisika.

3 Umewaonesha watu wako mazito,

Na kutunywesha mvinyo ya kutuyumbisha.

4 Isa 11:10 Umewapa wakuogopao bendera,

Ili itwekwe kwa ajili ya kweli.

5 Zab 108:6 Ili wapenzi wako waopolewe,

Utuokoe kwa mkono wako wa kulia, utuitikie.

6 Zab 89:35;Mwa 12:6;Yos 13:27 Mungu amenena kwa utakatifu wake,

Nami nikishangilia.

Nitaigawanya Shekemu,

Na kulipima bonde la Sukothi.

7 Kum 33:17;Mwa 49:10 Gileadi ni yangu, na Manase ni yangu,

Na Efraimu ni kinga ya kichwa changu.

Yuda ni fimbo yangu ya kifalme,

8 Moabu ni bakuli langu la kunawia.

Nitamtupia Edomu kiatu changu,

Na kumpigia Filisti kelele za vita.

9 Ni nani atakayenipeleka hadi mji wenye boma?

Ni nani atakayeniongoza hadi Edomu?

10 Zab 44:9 Ee Mungu, si Wewe uliyetutupa?

Wala, Ee Mungu, hutoki na majeshi yetu?

11 Utuletee msaada juu ya mtesi,

Maana wokovu wa binadamu haufai kitu.

12 1 Nya 19:13 Kwa msaada wa Mungu tutatenda makuu,

Maana Yeye atawakanyaga watesi wetu.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também