Sifa kwa maajabu ya Mungu
1 Haleluya.111:1 Haleluya: maana yake ni, Msifuni BWANA.
Nitamshukuru BWANA kwa moyo wangu wote,
Barazani pa wanyofu wa moyo na katika mkutano.
2 Ayu 38:1 Matendo ya BWANA ni makuu,
Yafikiriwa sana na wapendezwao nayo.
3 Kazi yake imejaa heshima na adhama,
Na haki yake yadumu milele.
4 Amefanya ukumbusho wa matendo yake ya ajabu;
BWANA ni mwenye fadhili na rehema.
5 Amewapa wamchao chakula;
Atalikumbuka agano lake milele.
6 Amewajulisha watu wake uwezo wa matendo yake,
Kwa kuwapa urithi wa mataifa.
7 Zab 19:7 Matendo ya mikono yake ni kweli na hukumu,
Maagizo yake yote ni amini,
8 Ufu 15:3 Yamethibitika milele na milele,
Yamefanywa kwa uaminifu na haki.
9 Ufu 15:3 Amewapelekea watu wake ukombozi,
Ameamuru agano lake liwe la milele,
Jina lake ni takatifu na la kuogopwa.
10 Kum 4:6;Ayu 28:28;Mit 1:7;9:10;Mhu 12:3 Kumcha BWANA ndio mwanzo wa hekima,
Wote wafanyao hayo wana ufahamu mzuri,
Sifa zake zadumu milele.