Sala ya ulinzi kutoka kwa adui
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.
1 Mungu, uisikie sauti yangu katika malalamiko yangu;
Unilinde uhai wangu kutoka kwa hofu ya adui.
2 Zab 143:9 Unifiche mbali na njama za watenda mabaya,
Mbali na mipango ya watu wafanyao maovu;
3 Zab 57:4 Waliounoa ulimi wao kama upanga,
Wanaoyalenga maneno ya uchungu kama mishale,
4 Wapate kumpiga mkamilifu faraghani,
Kwa ghafla humpiga bila kuogopa.
5 Walijifanya hodari katika jambo baya;
Hushauriana juu ya kutega mitego;
Wakisema, Ni nani atakayeiona?
6 Ni nani atambuaye maovu yetu?
Tumepanga njama kwa werevu mwingi,
Maana katika moyo wa mtu na fikira mengi yamefichika.64:6 Maana ya mstari huu si dhahiri kwa Kiebrania.
7 Lakini Mungu atawapiga kwa mshale wake,
Na kuwajeruhi ghafla.
8 Mit 12:13 Kwa ajili ya ulimi wao wataangamizwa;
Wote wawaonao watatetemeka kwa hofu.
Wote wawaonao watatikisa kichwa.
9 Na watu wote wataogopa,
Wataitangaza kazi ya Mungu,
Na kuyafahamu matendo yake.
10 Zab 32:11;Flp 4:4 Mwenye haki atamfurahia BWANA na kumkimbilia,
Na wote wenye moyo wa adili watasifu.