Sifa kwa mwamuzi wa Dunia
Zaburi.
1 Isa 59:16 Mwimbieni BWANA wimbo mpya,
Kwa maana ametenda mambo ya ajabu.
Mkono wa kulia,
Na mkono wake mtakatifu umemtendea wokovu.
2 Isa 52:10;Lk 2:30;Isa 62:2;Rum 3:25;Law 26:45;Kum 4:31;Mik 7:20;Lk 1:54;Isa 49:6;Lk 3:6;Mdo 13:47 BWANA ameufunua wokovu wake,
Machoni pa mataifa ameidhihirisha haki yake.
3 Amezikumbuka rehema zake,
Na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli.
Miisho yote ya dunia imeuona
Wokovu wa Mungu wetu.
4 Mshangilieni BWANA, nchi yote,
Inueni sauti, imbeni kwa furaha, imbeni sifa.
5 Mwimbieni BWANA sifa kwa kinubi,
Kwa kinubi na sauti tamu.
6 Hes 10:10;1 Nya 15:28;2 Nya 29:27 Kwa panda na sauti ya baragumu.
Shangilieni mbele za Mfalme, BWANA.
7 Bahari na ivume na vyote viijazavyo,
Ulimwengu nao wanaokaa ndani yake.
8 Mito na ipige makofi,
Milima na iimbe pamoja kwa furaha.
9 Mbele za BWANA;
Kwa maana anakuja kuihukumu nchi.
Atauhukumu ulimwengu kwa uaminifu,
Na mataifa kwa adili.