Publicidade

Salmos 39

Sala ya kutaka hekima na msamaha
Kwa mwimbishaji: kwa Yeduthuni. Zaburi ya Daudi.

1 Nilisema, Nitazitunza njia zangu

Nisije nikakosa kwa ulimi wangu;

Nitajitia lijamu kinywani,

Maadamu mtu mbaya awapo mbele yangu.

2 Nilikuwa sisemi, nilinyamaa kimya,

Sina faraja, maumivu yangu yakazidi.

3 Moyo wangu ukawa moto ndani yangu,

Na katika kuwaza kwangu moto ukawaka;

Nilisema kwa ulimi wangu,

4 BWANA, unijulishe mwisho wangu,

Na idadi ya siku zangu ni ngapi;

Nijue jinsi maisha yangu yalivyo mafupi.

5 Tazama, umefanya siku zangu kuwa mashubiri;

Maisha yangu ni kama si kitu mbele zako.

Kila mwanadamu, ingawa amesitawi, ni ubatili.

6 Kweli, watu wote hupita kama kivuli;

Wao hujisumbua bure tu;

Wanajirundikia mali wala hawajui ni nani atakayeirithi.

7 Na sasa ninangoja nini, Ee Bwana?

Matumaini yangu ni kwako.

8 Uniokoe kutoka kwa maasi yangu yote,

Usinifanye niwe wa kulaumiwa na mpumbavu.

9 Nimenyamaza, sifumbui kinywa changu,

Maana Wewe ndiwe uliyeyafanya.

10 Uniondolee pigo lako;

Kwa mapigo ya mkono wako nimeangamia.

11 Ukimrudi mtu kwa kumkemea kwa uovu wake,

Watowesha uzuri wake kama nondo.

Kila mwanadamu ni ubatili.

12 Ee BWANA, usikie maombi yangu,

Utege sikio lako niliapo,

Usiyapuuze machozi yangu.

Kwa maana mimi ni mgeni wako,

Msafiri kama baba zangu wote.

13 Uache kunitazama, ndio nipate kufurahi tena,

Kabla sijafa na kutoweka kabisa.

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-16_06-50-08-