Pular para o conteúdo
Publicidade

Zaburi 150

Sifa kwa ukuu Mwingi wa Mungu

1 Haleluya.

Msifuni Mungu katika patakatifu pake;

Msifuni katika anga la uweza wake.

2 Msifuni kwa matendo yake makuu;

Msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake.

3 Msifuni kwa mvumo wa baragumu;

Msifuni kwa kinanda na kinubi;

4 Kut 15:20;Isa 38:20 Msifuni kwa matari na kucheza;

Msifuni kwa zeze na filimbi;

5 Msifuni kwa matoazi yaliayo;

Msifuni kwa matoazi yavumayo sana.

6 Ufu 5:13 Kila mwenye pumzi na amsifu BWANA.

Haleluya.

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Veja também