Publicidade

Salmos 56

Kumtumaini Mungu katika mateso
Kwa mwimbishaji: kwa mtindo wa Njiwa Mkimya wa Mbali. Utenzi wa Daudi alipokamatwa na Wafilisti kule Gathi.

1 Mungu, unirehemu, maana yuko atakaye kunimeza,

Mchana kutwa ananionea akileta vita.

2 Adui zangu wanataka kunimeza mchana kutwa,

Maana ni wengi wanaonipiga vita.

3 Siku ya hofu yangu nitakutumaini Wewe;

4 Kwa msaada wa MUNGU nitalisifu neno lake.

Nimemtumaini Mungu, sitaogopa;

Mwenye mwili atanitenda nini?

5 Mchana kutwa wanapotosha maneno yangu,

Mawazo yao yote ni juu yangu kunitakia mabaya.

6 Hukutanika, hujificha, huziangalia nyayo zangu,

Kwa kuwa waliniotea ili waniue.

7 Je! Wataokoka kwa uovu wao?

Ee Mungu, uwaangamize kwa hasira yako.

8 Umehesabu kutangatanga kwangu;

Uyatie machozi yangu katika chupa yako;

(Je! Hayamo katika kitabu chako?)

9 Ndipo adui zangu watarudi nyuma siku ile niitapo.

Neno hili najua kuwa MUNGU yu upande wangu;

10 Kwa msaada wa MUNGU nitalisifu neno lake.

Kwa msaada wa BWANA nitalisifu neno lake.

11 Nimemtumaini Mungu, sitaogopa;

Mwanadamu atanitenda nini?

12 Ee Mungu, nadhiri zako ziko juu yangu;

Nitakutolea dhabihu za kushukuru.

13 Maana umeniponya nafsi yangu na mauti;

Je! Hukuizuia miguu yangu isianguke?

Ili niende mbele za Mungu

Katika nuru ya walio hai.

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-16_06-50-08-