1 BWANA akujibu siku ya dhiki,
Jina la Mungu wa Yakobo likuinue.
2 Akutumie msaada toka patakatifu pake,
Na kukutegemeza toka Sayuni.
3 Azikumbuke sadaka zako zote,
Na kuzitakabali dhabihu zako.
4 Akujalie kwa kadiri ya haja ya moyo wako,
Na kukutimizia mipango yako yote.
5 Na tuushangilie wokovu wako,
Kwa jina la Mungu wetu tuzitweke bendera zetu.
BWANA akutimizie matakwa yako yote.
6 Sasa najua kuwa BWANA amwokoa masihi wake;
Atamjibu toka mbingu zake takatifu,
Kwa matendo makuu ya wokovu
Ya mkono wake wa kulia.
7 Hawa wanataja magari na hawa farasi,
Lakini sisi tutalitaja jina la BWANA, Mungu wetu.
8 Wao wameinama na kuanguka,
Bali sisi tumeinuka na kusimama.
9 BWANA, umwokoe mfalme,
Utuitikie siku tuitayo.